Wikipedia ya Kiswahili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Wikipedia ya Kiswahili
Wikipedia-logo-v2-sw.svg
Ukurasa wa "Mwanzo" mwaka 2004

Wikipedia ya Kiswahili (au Wikipedia kwa Kiswahili) ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kiswahili.

Wikipedia kwa Kiswahili ilianzishwa mnamo tarehe 8 Machi 2003, na tarehe 1 Aprili, 2015, Wikipedia ya Kiswahili imefikia makala zipatazo 28,331 na kuifanya iwe Wikipedia ya 91 kwa hesabu ya makala zote.[1]

Kwa hesabu ya makala yenye zaidi ya herufi 200 (yaani bila makala mafupi mno) imefikia nafasi ya 71. [2]

Maendeleo[hariri | hariri chanzo]

Ilipofika tarehe 26 Septemba 2007, Wikipedia ya Kiswahili ilifikisha makala 6,000.

Mnamo tarehe 21 Aprili 2008, Wikipedia ya Kiswahili ilifikisha makala 7,000.

Ilipofika tarehe 19 Desemba 2008, Wikipedia ya Kiswahili ilifikisha makala 8,000, hasa baada ya kuanzishwa makala nyingi za mbegu za kata za Tanzania.

Makala za mbegu ya Tanzania, ziliendelea kuisukuma Wikipedia ya Kiswahili hadi kufikia kiwango cha makala 9,000 na hiyo ilikuwa kunako tarehe 2 Februari 2009.

Mbegu ziliendelea hadi kufikia makala 10,000 mnamo tarehe 21 Februari 2009.

Ilipofika tarehe 9 Aprili 2009, Wikipedia ya Kiswahili ilifikia kiwango cha makala 11,000.

Kunako tarehe 25 Aprili 2009, Wikipedia ya Kiswahili ilifikia makala 12,000.

Mnamo tarehe 20 Juni 2009, Wikipedia ya Kiswahili imebadilisha ukurasa wake wa mwanzo katika sura mpya.

Mnamo tarehe 17 Agosti 2009, Wikipedia ya Kiswahili ilifikia makala zipatazo 13,000, na kuendelea kuifanya iwe Wikipedia ya kwanza kwa ukubwa katika Afrika.

Haikushia hapo na ilivyofika tarehe 11 Septemba 2009, Wikipedia hii ilifikia makala 14,000.

Tarehe 15 Februari 2014 ilifikia makala 26,000 na tarehe 28 Oktoba mwaka huohuo makala 27,000.

Tarehe 25 Januari 2015 ilivuka idadi ya makala 28,000.

Kati ya Wikipedia za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Katika Afrika na visiwa vya jirani, Wikipedia kwa Kiswahili ndiyo ya nne kwa idadi ya makala zote ikifuatia Wikipedia ya Kimalagasy, Wikipedia ya Kiyoruba na Wikipedia ya Kiafrikaans. Kwa kuangalia yaliyomo halisi (bila makala mafupi sana) ndiyo ya pili baada ya Kiafrikaans.

Pia, ndiyo ya kwanza kati ya Wikipedia za lugha za Niger-Kongo kuvuka kiwango cha makala 1,000.

Wikipedia kwa Kiswahili, ndiyo ya pili katika Afrika kuvuka kiasi cha makala 10,000 baada ya Wikipedia ya Kiafrikaans. [3]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]