Ukanda wa Gaza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Ukanda wa Gaza.

Ukanda wa Gaza ni eneo dogo kwenye mwambao wa Mediteranea ya Mashariki lililopo sehemu ya Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina ya Palestina. Lina urefu wa kilomita 40 na upana kati ya km 6 na 14. Eneo lote halizidi km² 360. Gaza imepakana na Bahari ya Kati halafu nchi za Israel (upande wa mashariki na kaskazini) na Misri (upande wa kusini-magharibi). Israeli inatenganisha Gaza na maeneo upande wa magharibi ya mto Yordani yaliyo pia chini ya mamlaka ya Palestina.

Ni kati ya maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu likiwa na wakazi milioni 1.4 yaani zaidi ya watu 4,100 kwa km².

Mji mkubwa ni Gaza.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ukanda huu ni kati ya mabaki ya Palestina ya Kiingereza yasiyotwaliwa na Israeli wakati wa vita ya Kiarabu-Kisraeli ya 1948 na kuwa kimbilio kwa wakimbizi wengi Wapalestina waliowahi kukaa katika sehemu zilizopata kuwa za Israeli. Kati ya miaka 1948 hadi 1967 ulitawaliwa na Misri. Tangu vita ya siku sita ya 1967 ulikuwa chini ya Israeli.

Tangu mwaka 1994 ulikabidhiwa kwa mamlaka ya Palestina lakini Israeli iliendelea kuwa na vijiji vya Waisraeli na vituo vya kijeshi ndani yake. Mapigano ya intifada yaliongezeka kuwa makali na kusababisha vifo vingi. Tangu mwaka 2005 Israeli iliondoa wakazi na wanajeshi wake wote.

Baada ya uchaguzi wa 2006 chama cha Hamas chini ya Ismael Haniya kilipata kura nyingi na kushika serikali ya Palestina. Farakano kati ya Hamas na Fatah wa rais Mahmud Abas liliongezeka hadi Hamas kuchukua mamlaka yote katika Gaza kwa nguvu ya silaha mwezi wa Juni 2007. Tangu mwezi ule Gaza iko chini ya serikali ya Hamas lakini maeneo mengine yako chini ya mamlaka ya rais Abas.

Hali ya maisha ya wakazi wake ni ngumu. Israeli imefunga mipaka na kuzuia wakazi wa Gaza wasitoke nje kwa sababu wanamgambo Wapalestina wanaendelea kurusha roketi ndogo kutoka Gaza kwenda Israeli. Kutokana na kufungwa kwa mipaka yote uchumi ni duni: hakuna ajira. Hata huduma za msingi kama vile maji na umeme zinavurugika kabisa.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ukanda wa Gaza kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.