Nenda kwa yaliyomo

Kitabu cha Hagai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kitabu cha Hagai ni kimojawapo kati ya vitabu 12 vya Manabii wadogo ambavyo, pamoja na vingine vingi, vinaunda Tanakh, yaani Biblia ya Kiebrania. Hivyo ni pia sehemu ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mwandishi na muda

[hariri | hariri chanzo]

Kazi ya nabii huyo kati ya Agosti na Desemba ya mwaka 520 KK, wakati uleule alipoanza nabii Zekaria, ni mwanzo wa kipindi cha mwisho cha unabii katika Israeli kabla ya ujio wa Yohane Mbatizaji na Yesu Kristo.

Mazingira

[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya uhamisho wa Babeli, ujumbe wa manabii ulitishia mara nyingi adhabu ya Mungu kwa uasi wa taifa lake.

Wakati wa uhamisho ujumbe ulikuwa wa faraja zaidi.

Ule wa Hagai na Zekaria ulilenga ustawi wa Wayahudi waliokuwa wamerudi Yerusalemu mwaka 538 K.K. ili kujenga upya hekalu, lakini walichelewa kutekeleza azma yao, kutokana na upinzani na mahangaiko ya kujipatia riziki katika mazingira magumu.

Mbaya zaidi, walikaribia kukata tamaa. Kwa changamoto ya manabii wao, gavana Zerubabeli na kuhani mkuu Yoshua waliongoza wananchi kukazania ujenzi huo na kuukamilisha mwaka 515 KK.

Muhtasari

[hariri | hariri chanzo]

Juhudi hizo ndizo lengo la hotuba zote nne zinazounda kitabu hiki, ambapo ujenzi wa hekalu ni sharti la ujio wa ufalme wa Mungu.

Ahadi ya kuwa hatimaye hekalu jipya litakuwa tukufu kuliko lile la Solomoni ni la maana zaidi kwa Wakristo wanaoiona kama utabiri wa Yesu mfufuka, aliye hekalu la kweli la Agano Jipya (Yoh 2:19-22).

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Hagai kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.