Nenda kwa yaliyomo

Wimbo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lady Jay Dee, mwanamuziki wa Bongo Flava

Wimbo/nyimbo ni tungo zenye kufuata mapigo fulani ya kimi za kiafuziki yenye mahadhi ya kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti (urari wa sauti) na mpangilio maalumu wa maneno.

Nyimbo huundwa kwa lugha ya mkato na matumizi ya lugha ya picha (taswira).

Muundo wa nyimbo huwa ni wa kuimbika na mizani ya kila mstari mara nyingi huwa inalingana.

Wahusika wa nyimbo huwa ni mtu mmoja au kikundi cha watu. Nyimbo aghalabu huambatana na ala za muziki kama vile ngoma, zeze, marimba, makofi, vigelegele na kadhalika.

Mashairi ya nyimbo huimbwa popote pale panapostahili kulingana na tukio au muktadha unaofungamana na wimbo. Hivyo basi kuna nyimbo za dini, harusi, siasa, jando/unyago, kilimo, nyimbo za kuwinda na kadhalika.

  • Nyimbo za wanabaharia huitwa kimai.
  • Nyimbo za kulika huitwa wawe au vave.
  • Nyimbo ziimbwazo mja anapofanya kazi huitwa hodiya.
  • Nyimbo ziimbwazo na watoto wanapocheza huitwa Nyimbo za chekechea.
  • Nyimbo ziimbwazo ili kuwabembeleza watoto huitwa bembeleza au bembezi.

Aina za nyimbo

[hariri | hariri chanzo]

Kuna aina nyingi za nyimbo zikitofautishwa na nchi, utamaduni na waimbaji wenyewe. Kwa mfano kuna nyimbo za kitamaduni, za Kiinjili na za kisasa.

Hivyo vikundi ni kulingana na nyakati na vinaweza kugawanywa zaidi kulingana na tofauti. Kwa mfano nyimbo za kisasa zinaweza kugawanywa kulingana na mtindo wa wimbo. Nyimbo zinaweza kugawanywa kulingana na nchi. Nchini Kenya kuna nyimbo za makabila tofautitofauti kama chakacha na mugithi ambazo zinahusishwa na kabila tofautitofauti.

Nyimbo za kisasa zinarekodiwa kwenye studio za kisasa lakini pia katika studio za nyumbani, mtindo unaoleta mageuzi makuu kwa wasanii. Leo unaweza kurekodi wimbo mzima ukiwa nyumbani mradi uwe na vifaa vinavyohitajika.

Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wimbo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.