Nenda kwa yaliyomo

Mpanda (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wilaya ya Mpanda Mjini)
Ramani ya mkoa wa Katavi (kijani cheusi), Tanzania

Mpanda ni makao makuu na pia mji mkubwa wa Mkoa wa Katavi katika magharibi ya Tanzania.

Ni kitovu muhimu cha biashara ya mazao kama mahindi na mpunga; kuna pia dalili ya uchumi wa madini, hasa dhahabu, katika mazingira yake.

Mji umekua sana kuanzia wakazi 46,000 mwaka 2002 hadi kufikia idadi ya wakazi 102,000 wakati wa sensa ya mwaka 2012 na 245,764 katika ile ya mwaka 2022 [1].

Hadi mwaka 2014 hapakuwa na barabara za lami bali njia za udongo pekee, hivyo usafiri ulikuwa na shida wakati wa mvua. Kuna njia ya reli kutoka huko hadi Kaliua inapoungana na Reli ya Kati. Safari ya reli hadi Tabora inachukua masaa 10 - 12. Mabasi yanakwenda kila siku Sumbawanga (masaa 5), Mbeya na Tabora (masaa 9). Baada ya kuwa makao makuu ya mkoa wa Katavi uwanja wa ndege uliboreshwa mwaka 2012.

Upande wa dini kuna makao makuu ya dayosisi ya Kikatoliki pamoja na dayosisi ya Anglikana ya Ziwa Rukwa na makanisa ya Moravian, AIC, Wapentekoste na pia misikiti mbalimbali.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ilianzishwa mnamo mwaka 1983 ndani ya mkoa wa Rukwa. Mnamo mwaka 2012 wilaya hii iligawanywa na kupata wilaya ya Mlele na Mpanda yenyewe. Mkoa wa Katavi ulianzishwa mwaka 2012 baada ya kuigawanya Halmashauri hii na kupata wilaya tatu (3) na halmashauri za wilaya tano (5). Wilaya hizo ni wilaya ya Mpanda ambayo ina halmashauri za wilaya mbili (2) ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo. [2]

Kata za Wilaya ya Mpanda MjiniMkoa wa Katavi - Tanzania

Ilembo | Kakese | Kashaulili | Kasokola | Kawajense | Kazima | Magamba | Majengo | Makanyagio | Misunkumilo | Mpanda Hotel | Mwamkulu | Nsemulwa | Shanwe | Uwanja wa Ndege


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Katavi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.