Mpanda (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mpanda ni makao makuu na pia mji mkubwa wa Mkoa wa Katavi katika magharibi ya Tanzania. Ni kitovu muhimu cha biashara ya mazao kama mahindi na mpunga kuna pia dalili ya uchumi wa madini hasa dhahabu katika mazingira yake.

Mji umekua sana kuanzia wakazi 46,000 mwaka 2002 hadi kufikia idadi ya wakazi 102,000 wakati wa sensa ya 2012. [1]

Hadi mwaka 2014 hapakuwa na barabara za lami bali njia za udongo pekee hivyo usafiri huwa na shida wakati wa mvua. Kuna njia ya reli kutoka hapa hadi Kaliua inapoungana na Reli ya Kati. Safari ya reli hadi Tabora inachukua masaa 10 - 12. Mabasi yanaenda kila siku Sumbawanga (masaa 5), Mbeya na Tabora (masaa 9). Tangu kuwa makao makuu ya mkoa wa Katavi uwanja wa ndege uliboreshwa mwaka 2012.

Upande wa dini kuna makao makuu ya dayosisi wa Kikatoliki pamoja na dayosisi ya Anglika ya Ziwa Rukwa na makanisa ya Moravian, AIC, Assemblies na pia msikiti mbalimbali.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Mpanda Mjini - Mkoa wa Katavi - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Ilembo | Kakese | Kashaulili | Kawajense | Makanyagio | Misunkumilo | Mpanda Hotel | Nsemulwa | Shanwe