When You Tell Me That You Love Me

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“When You Tell Me That You Love Me”
“When You Tell Me That You Love Me” cover
Single ya Diana Ross
Muundo CD, Vinyl (7" & 12")
Aina Soul
Urefu 4:14
Studio Motown
Mtayarishaji Peter Asher
Mwenendo wa single za Diana Ross
"No Matter What You Do"
(1991)
"When You Tell Me That You Love Me"
(1991)
"The Force Behind The Power"
(1991)

"When You Tell Me That You Love Me" ni wimbo uliotoka kama single mwaka 1991 kutoka kwa mwanamuziki wa nchini Marekani anayeitwa Diana Ross. Baadaye wimbo huu ulirudiwa kuimbwa na wanamuziki mbalimbali.

"When You Tell Me That You Love Me" ilikuwa ni single ilioongoza kutoka kwa albamu ya Diana Rose iliyotoka mwaka 1991, iliyoitwa The Force Behind the Power iliyotolewa na studio Motown nchini Marekani, na stdudio ya EMI ya nchini Uingereza.Wimbo huu wa mapenzi lakini yanayosikitisha ndio uliofanya vizuri zaidi katika albamu hii. Wimbo huu uliweza kufika nafasi ya 37# katika chati ya muziki ya Marekani ya Billboard na kushika nafasi ya 2# katika single 75 bora nchini Uingereza.Rose anauchukulia wimbo huu kama wimbo wenye kumatambulisha. [1] Toleo la nchini Uingereza lilijumuisha wimbo wake uliofanya vizuri mwaka anaoitwa "Chain Reaction." [2]

Muziki wa Video[hariri | hariri chanzo]

Video ya muziki huu ilitoka ikiwaonesha Ross akiwa katika gauni la jioni, akiwa anaimba katika jukwaa, na kuingiza picha zingine zikimwonesha Ross akiwa na watoto wake wawili wa kiume, Ross & Evan. [3]

Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

UK Vinyl, 12" (12 EM 217)[4]

 1. When You Tell Me That You Love Me (LP Version) (4:14)
 2. Chain Reaction (12" Version) (3:50)
 3. You And I (4:06)

UK CD Maxi (CDEM 217, 20 5600 2 )[5]

 1. When You Tell Me That You Love Me (LP Version) (4:14)
 2. Chain Reaction (12" Version) (3:50)
 3. You And I (4:06)

US Vinyl, 12" (L33-1643 )[6]

 1. When You Tell Me That You Love Me (LP Version) (4:10)
 2. When You Tell Me That You Love Me (LP Version) (4:10)

US Cassette Single" (MOTCS-2139 )[6]

 1. When You Tell Me That You Love Me (LP Version) (4:10)

Chati[hariri | hariri chanzo]

Chati (1991) Ilipata
nafasi
UK Singles Chart 2
Hot R&B/Hip-Hop Songs 37

Toleo la Julio Iglesias[hariri | hariri chanzo]

“When You Tell Me That You Love Me”
“When You Tell Me That You Love Me” cover
Single ya Julio Iglesias na Dolly Parton
Muundo 5" CD Single
Aina Pop, soul
Urefu 3:59
Studio Columbia Records
Mtunzi Albert Hammond na Bettis

Wimbo huu ulirekodiwa tena, kwa Dolly Parton kushirikiana na Julio Iglesias kwa ajili ya lalbamu yao ya mwaka 1994 iliyoitwa Crazy. Single hii ilitoka mwaka 1995 na kufanikiwa kuingia katika chati ya muziki ya Uholanzi na kukaa kwa kipindi cha takribani wiki tatu. Wimbo huu uliingia katika chati hii na kushika nafasi ya 48# na baadae nafasi ya 45# la mwishoni ilishika nafasi ya 49# [7]

Kwa mujibu wa Iglesias, Parton alikuwa mmoja kati ya wanamuziki aliopenda kufanya nao kazi. Parton alijumuisha wimbo huu katika diski yake ya The Tour Collection. [8]

Miziki wa Video[hariri | hariri chanzo]

Video ya muziki ilifanyika katika Jumba la Oheka lililipo katika kisiwa cha Long Island kaskazini mwa ufukwe wa bahari. Katika toleo lingine, Iglesias na Parton wanaonekana kuimba katika vyumba tofauti tofauti, la hali ya mapenzi kuwatawala. Mwishoni mwa video anaonekana Parton na Iglesias wakiwa wanatoka katika jumba hilo, huku Parton akiwa amebadilisha kutoka gauni lenye rangi jeupe kwenda gauni jeusi[9]

Chati[hariri | hariri chanzo]

Chati (1995) Ilipata
nafasi
Dutch Top 40[7] 45

Toleo na CoCo Lee[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1998 Iglesias alirudia kurekodi wimbo huo na mwanamuziki kutoka nchini China anayeitwa Coco Lee (李玟) ulitoka kama single katika kutangaza mkusanyiko wake wa nyimbo zilizoitwa My Life: The Greatest Hits. lakini pamoja na haya, toleo la Coco halikujumuishwa katika albamu yake na badala yake likajuimshwa lile la Parton. [10] Video ya Muziki ilitoka ikimwonesha Iglesias na Lee wakiwa katika studio ya kurekodia. mwishoni, Iglesias na Lee wanaonekana wakiwa wamekaa katika chakula cha jioni. [11]

Toleo la Westlife[hariri | hariri chanzo]

“When You Tell Me That You Love Me”
“When You Tell Me That You Love Me” cover
Single ya Westlife and Diana Ross
kutoka katika albamu ya Face To Face
Muundo CD Single
Aina Pop, soul
Studio Sony BMG
Certification Silver
"You Raise Me Up"
(1)
"When You Tell Me That You Love Me"
(2)
"Amazing"
(3)

Diana Ross alirekodi kwa mara ya pili wombo wake wa When You Tell Me That You Love Me na kundi kutoka nchini Ireland la Westlife, mwaka 2005 katika albamu yao inayoitwa Face To Face Ilikuwa ni single ya pili katika albamu hii. Wimbo huu ulishika nafasi ya thelathini na tisa katika nyimbo zilizoongoza kwa mauzo nchini Uingereza kwa mwaka 2005

Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

CD ya kwanza[hariri | hariri chanzo]

 1. When You Tell Me That You Love Me (With Diana Ross) (Single Mix)
 2. White Christmas
 3. The Way You Look Tonight (Westlife Only Version)

CD ya pili[hariri | hariri chanzo]

 1. When You Tell Me That You Love Me (With Diana Ross) (Single Mix)
 2. If I Let You Go (Acoustic Version)

Chati[hariri | hariri chanzo]

Chati (2005) Ulipata
nafasi
Dutch Top 40[12] 45
Irish Singles Chart 2
UK Singles Chart 2

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]