Diana Ross

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Diana Ross
Diana Ross akiimba kwenye sherehe ya 2008 Nobel Peace Prize mjini Oslo
Diana Ross akiimba kwenye sherehe ya 2008 Nobel Peace Prize mjini Oslo
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Diana Ernestine Earle Ross
Amezaliwa 26 Machi 1944 (1944-03-26) (umri 79)
Asili yake Detroit, Michigan, Marekani
Aina ya muziki R&B, soul, disco, jazz
Kazi yake Mwimbaji, mtayarishaji wa rekodi, mwigizaji
Aina ya sauti Soprano[1]
Miaka ya kazi 1959–mpaka sasa
Studio Lu Pine, Motown, RCA, EMI
Ame/Wameshirikiana na The Supremes,Mary Wilson,Florence Ballard, Marvin Gaye, The Jackson 5, Michael Jackson, Lionel Richie, Chic, The Temptations, Ashford & Simpson
Tovuti www.dianaross.com

Diana Ernestine Earle Ross (amezaliwa tar. 26 Machi 1944) ni mwimbaji na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Kwenye miaka ya 1960, ameisaidia kuumbisha midundo ya Motown akiwa kama mwimbaji kiongozi wa The Supremes, kabla hajaondoka kundini kwa ajili ya kufanyakazi za kujitemea hapo 14 Januari 1970. Tangu kuanza kazi zake za kimuiziki akiwa na The Supremes na kama msanii wa kujitegemea, Ross ameuza zaidi ya rekodi milioni 150.[2]

Kwenye miaka ya 1970 hadi katikati mwa miaka ya 1980, Ross alikuwa miongoni mwa wasanii wa kike wenye mafanikio makubwa kabisa, katika nyanja za filamu, televisheni na hata Broadway. Alipata kuchaguliwa kama Best Actress Academy Award kwa mwaka wa 1972 alivyocheza kama Billie Holiday kwenye filamu ya Lady Sings the Blues, ambayo pia ameshinda tuzo ya Golden Globe. Ameshinda matuzo kadhaa kwenye American Music Award, amechaguliwa mara kumi na mbili kwenyye Grammy Award, na kushinda Tony Award kwa ajili ya kipindi chake cha mwanamke mmoja, An Evening with Diana Ross, mnamo mwaka wa 1977.

Mwaka wa 1976, jarida la Billboard wamemwita "Mburudishaji wa Kike wa Karne." Mwaka wa 1993, kina Guinness Book of World Records wamemtangaza Diana Ross msanii wa kike mwenye mafanikio zaidi katika historia ya muziki akiwa na jumla vibao vikali 18 vikiwa nafasi ya kwanza huko nchini Marekani: 12 akiwa kama mwimbaji mkuu wa The Supremes na sita akiwa kama msanii wa kujitegemea. Ross alikuwa msanii wa kwanza mwanamke kushinda vibao vikali sita vikiwa nafasi ya kwanza. Ushirika huu unamweka nafasi ya tano katika wasanii wa kike wa kujitegemea kuwa na vibao vingi vya nafasi ya kwanza kwenyer Hot 100.[3] Pia ni mmoja kati ya wasanii wachache wa rekodi kuwa na nyota mbili kwenye Hollywood Walk of Fame—moja akiwa kama msanii wa kujitegemea na nyingine akiwa kama mwanachama wa The Supremes. Mwezi wa Desemba 2007, amepokea Tuzo ya Heshima ya John F. Kennedy Center for the Performing Arts .

Ukijumlisha na kazi zake alizofanya na The Supremes, Ross ametoa jumla ya albamu zipatazo 67.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Diskografia ya kujitegemea[hariri | hariri chanzo]

Singe za Kumi Bora[hariri | hariri chanzo]

Single zifuatazo zimefika katika Kumi Bora aidha kwenye chati za pop za Billboard Hot 100 nchini Marekani au UK Singles Chart huko nchini Uingereza.

Top Ten albums[hariri | hariri chanzo]

Albamu zifuatazo zimefikia katika Kumi Bora ya chati za albamu aidha nchini Marekani, ikiwa ni pamoja na chati za R&B au chati za albamu za pop huko nchini Uingereza.

Filmografia[hariri | hariri chanzo]

Televisheni[hariri | hariri chanzo]

  • 1968: [Tarzan (TV Series)] (akiwa na The Supremes)
  • 1968: T.C.B. (akiwa na The Supremes)
  • 1969: G.I.T. on Broadway (akiwa na The Supremes)
  • 1971: Diana!
  • 1977: The Big Event: An Evening with Diana Ross
  • 1979: Diana Ross in Concert!
  • 1981: diana
  • 1981: Standing Room Only: Diana Ross
  • 1983: Motown 25: Yesterday, Today, Forever
  • 1983: For One And For All - Diana Ross Live! in Central Park
  • 1987: Diana Ross: Red Hot Rhythm and Blues
  • 1989: Diana Ross: Workin' Overtime
  • 1992: Diana Ross Live! The Lady Sings... Jazz & Blues: Stolen Moments
  • 1994: Out of Darkness
  • 1996: Super Bowl XXX
  • 1999: Double Platinum
  • 2000: VH1 Divas 2000: A Tribute to Diana Ross
  • 2005: Tsunami Aid
  • 2007: BET Awards 2007
  • 2007: Kennedy Center Honors
  • 2008: Nobel Peace Prize Concert

Tawasifu zake[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Dean, Maury (2003). Rock-N-Roll Gold Rush. Algora Publishing. p. 34. ISBN 0875862071. 
  2. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-03-15. Iliwekwa mnamo 2009-03-15.
  3. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-10-11. Iliwekwa mnamo 2008-10-11.

http://sixmillionsteps.com/drupal/node/1085 - 80 minute audio mix of Diana Ross songs/interviews

Soma zaidi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]