Nenda kwa yaliyomo

Broadway

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Broadway ya Manhattan, New York; matangazo mengi ya maigizo yanapamba nyumba zake.

Broadway ni jina la barabara katika miji mbalimbali hasa nchini Marekani. Maana ya jina ni "njia pana". Maarufu ni hasa Broadway mjini New York inayopita katika mitaa ya Manhattan na Bronx. Imekuwa maarufu hasa kutokana na kuwepo kwa jukwaa 40 za maigizo. Maonyesho mengi ya maigizo mashuhuri yalitokea hapo.