Jazz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Louis Armstrong aliyeitwa "Mfalme wa Jazz"
Bendi ya King & Carter Jazzing Orchestra ilikuwa kati ya kindi za kwanza za Jazz mjini Houston Texas

Jazz ni aina ya muziki iliyoanzishwa nchini Marekani. Jazz huunganisha tabia za muziki ya Kiafrika pamoja na tabia za muziki ya Ulaya.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Jazz ilianza mnamo mwanzo wa karne ya 20 Marekani. Kati ya vyanzo vyake ni muziki ya wamarekani weusi waliowahi kutunza muziki ya kiafrika kati yao kutokana na mababu waliopelekwa kama watumwa kutoka nchi za Afrika Magharibi. Pamoja na hayo walitumia pia sehemu za muziki ya Wamarekani wazungu yenye asili ya pande mbalimbali za Ulaya. Watalaamu kadhaa huitwa muziki yenye sauti ya Kiulaya pamoja na mpigo wa Kiafrika.

Neno la "jazz" kwa muziki ilitokea mara ya kwanza mjini New Orleans iliyoenea kutoka hapa katika maeneo jirani na miji mikubwa ya Marekani. Staili ya kusini ya Marekani iliitwa wakati ule "dixiland" kutokana na jina kwa ajili ya kusini ya nchi hii.

Kutoka asili hizi kuna aina nyingi za jazz zilizoendelea.

Wanamuziki mashuhuri[hariri | hariri chanzo]

Wanamuziki muhimu wa Jazz ni pamoja na:

Wapiga tarumpeta:

Wapiga saxophone:

Wapiga trombone:

Wapiga klarineti:

Wapiga piano:

Wapiga gitaa:

Wapiga ngoma

Waimbaji