Ella Fitzgerald

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ella Fitzgerald
Ella Fitzgerald mnamo 1946
Ella Fitzgerald mnamo 1946
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Ella Jane Fitzgerald
Amezaliwa 25 Aprili 1917 (1917-04-25) (umri 106)
Kazi yake Mwimbaji, mwigizaji, mwanamuziki
Ala Sauti
Miaka ya kazi 1934-1994
Studio Capitol Records
Tovuti ellafitzgerald.com


Ella Fitzgerald (25 Aprili 191715 Juni 1996) alifahamika kama muimbaji wa kike wa muziki wa Jazz (Lady of songs). Ella Fitzgerald au mama Ella sauti yake ilikuwa ni muhimu sana kwenye muziki wa Jazz na hata mitindo mingine ya muziki katika karne ya ishirini.

Ella Fitzgerald alizaliwa 25 Aprili 1917 mjini Newport News (Va- Marekani). Ella ameshirikiana na wanamuziki wengi mojawapo ni Louis Armstrong "Satchimo" huyu alikuwa ni mpiga tarumpeta mashuhuri. Mama Ella alizama zaidi katika mtindo wa Swing Jazz.

Kati ya nyimbo alizowahi kuimba ni: That old black magic; Can't we be friends?; Love is the thing so they say; It's a blue wold; Dedicated to you; If you ever should live na Sugar blues. Alifariki mwaka 1996.