What Makes a Man

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“What Makes a Man”
“What Makes a Man” cover
Single ya Westlife
Muundo CD Single
Aina Pop
Mtunzi Wayne Hector, Steve Mac
Mwenendo wa single za Westlife
"My Love"
(2000)
What Makes A Man
(2000)

"What Makes a Man" ni wimbo wa Westlife, uliotoka kama single katika albamu yao ya Coast to Coast. Ilikuwa ni single yao ya kwanza kushindwa kufika katika nafasi ya kwanza katika chati ya Muziki ya Uingereza. Hali hii ikakifanya kikundi hichi kushindwa kuwa na nyimbo ya pili mfululizo katika nafasi ya kwanza katika nyimbo za Christmas. Wimbo uliokuwa umeshika nafasi hiyo ulikuwa wimbo wa "Can We Fix It" ulioimbwa na Bob the Builder. Wimbo wa Westlife ulishika nafasi ya 39 katika mauzo nchini Uingereza kwa kufanikiwa kuuza nakala 400,000 kwa mwaka 2000

Orodha ya Nyimbo[hariri | hariri chanzo]

CD ya kwanza[hariri | hariri chanzo]

  1. What Makes a Man (Single Remix)
  2. I'll Be There
  3. My Girl

CD ya pili[hariri | hariri chanzo]

  1. What Makes a Man (Single Remix)
  2. I'll Be There
  3. What Becomes of the Brokenhearted

Orodha ya matamasha[hariri | hariri chanzo]

Japokuwa wimbo huu haukufika katika nafasi ya kwanza, ulifanikiwa kuuza nakala 230,747 na kufika katika nafasi ya pili katika chati ya Nchini Uingereza, lakini kabla ya Christmas ulishindwa kutoa wimbo wa Bob The Builder na "Can we Fix It" kutoka katika nafasi ya kwanza.Wimbo huu ulifanikiwa kuuza zaidi katika wiki ya kwanza zaidi kuliko nyimbo nyingine hata wimbo wa "Uptown Girl". Ni wimbo wa tatu kuongoza kwa upande wa mauzo katika kundi ilo nchini Uingereza kwa kuuza nakala 390,407, na pia ni moja kati ya nyimbo zilizofanya vizuri kwa upande wa mauzo katika karne ya 21.

Katika nyimbo 100 bora, wimbo huu ulishika nafasi ya 87, na pia umefanikiwa kuuza zaidi ya nakala 400,000 nchini Uingereza pekee.

Chati Ilipata<>nafasi
Ireland 2
United Kingdom 2

Viunga vya nje[hariri | hariri chanzo]