Nenda kwa yaliyomo

Mark Feehily

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mark Feehily
Mark Feehily
Mark Feehily
Maelezo ya awali
Amezaliwa 28 Mei 1980 (1980-05-28) (umri 44)
Sligo, Ireland
Aina ya muziki Pop
Ala Vocals, piano.
Aina ya sauti Tenor
Miaka ya kazi 1998–present
Ame/Wameshirikiana na Westlife
Tovuti www.westlife.com


Mark Michael Patrick Feehily (amezaliwa tar. 28 Mei 1980 mjini Sligo, Ireland) ni msanii wa muziki wa pop kutoka nchini Ireland. Kijana huyu anajulikana zaidi kama Mark Feehily moja kati ya vijana ambao kwa pamoja huunda kundi la Westlife.

Mark ana wadogo zake wawili, Barry aliyezaliwa mwaka 19985 na Colin aliyezaliwa mwaka 1989. Wazazi wake ni Marie and Oliver Feehily.[1]

Katika kundi la Westlife Mark anatambulika kwa sauti yake nzito na hivyo imesikika katika nyimbo mbalimbali hasa katika viitikio na shairi la kwanza, na mara kadhaa akishirikiana na Shane Filan

Kabla ya kujiunga na kundi la Westlife, Shane Filan na Kian Egan walikuwa katika kundi la IOU ambapo ameshiriki katika utunzi wa nyimbo mbalimbali kama vile, Everlasting Love naTogether Girl Forever.

Feehily pia ameshirika katika kutunga nyimbo kadhaa za kundi la Westlife kama vile :[2]

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
  • Imaginary Diva
  • Reason For Living
  • Crying Girl
  • You Don't Know
  • Never Knew I Was Losing You
  • Where We Belong
  • Singing Forever
  • I Won't Let You Down
  • You See Friends (I See Lovers)
  • I'm Missing Loving You
  • Miss You When I'm Dreaming
  • Reach Out

Maisha Binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Feehily anajulikana kwa watu wengi kuwa ni shoga. Hii ikiwa imetangazwa katika gazeti la Udaku la Uingereza la The Sun, na ametangaza uhusiano wake wa muda mrefu na Kevin McDaid, mwimbaji wa kundi la Uingereza la wavulana V.[3][4] Katika mahojiano alisema "Maisha yangu yamekuwa bora zaidi, maisha yangu ya kimapezi hayawezi kunielezea mimi kama mtu, lakini ni kitu kikubwa kwa mtu yetote kuwa wazi kuhusiana nayo, imebadilisha maisha yangu moja kwa moja, najisikia mwenye furaha na mwepesi zaidi, Hiki ni kitu bora zaidi ambacho nimewahi kufanya" Tofauti na wenzake katika bendi hii, Freehili hapendi kuongelea maswala yake ya mahusiano. Mkurugenzi wake Louis Walsh anasema, wakati anamchagua hakujua kuhusu maisha yake binafsi.[5]

Wawili hawa wamekuwa katika mahusiano tangu Januari 005, walipokutana katika tamasha la Childline lililofanyika nchini Ireland. Alipohijiwa katika mahojiano mengine, Feehili aliliambia gazeti la Sydney Morning Herald Kuwa japokuwa mashabiki wa kundi hili wngi wao ni wasichana, hakujawa na mapokeo mabaya, anasema "Nia furaha sana sasa, na ninadhani hata mashabiki wetu wanaona hili" anasema "Katika miaka kadhaa hadi kufika hapa nilipo sasa, nilikuwa tayari kupitia katika mambo kadhaa kuhusiana na hisia zangu, lakini naweza kusema wazi kuwa, siku niliyoweza kukabiliana na woga huo, sikujali maekeo yake yangekuwa vipi, na hii ndio ilikuwa sehemu ngumu zaidi"

Feehily anasema kuwa, japo hajatarajia kufunga ndoa sasa, lakini ana furaha kujua kuwa, ataweza kufunga ndoa pindi atakapohitaji kufanya hivyo, ikiwa ni ndoa ya kiserikali [6] Wasema muda ukifika,wataweza kuangalia na kuoanga jinsi ya kufunga ndoa ya kiserikali

Mwezi Desemba mwaka 2007, Mark na Kevin walitokea katika ukurasa wa juu wa gazeti la Atitude, ambapo pia walifanya mahojiano. Katika mahojiano hayo Mark alisema kuwa anataka kuzeeka akiwa nae, na ana imani kuwa watakuwa pamoja daima.

  1. Mark Feehily bio on IMDB.com
  2. http://www.thecommitted.com/cgi-bin/index.cgi?action=forum&board=MP3s&op=displaysticky&num=11984
  3. Victoria Newton. "Mark: I'm so glad I came out" (Website) (kwa English). The Sun. Iliwekwa mnamo 2007-12-22.{{cite web}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
  4. Westlife singer reveals 'I'm gay', BBC News Online, 19 Agosti 2005
  5. "Louis 'mightn't have picked' gay Gately". Irish Independent. 2008-11-23. Iliwekwa mnamo 2008-11-25. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help)
  6. Sydney Morning Herald

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]