Nenda kwa yaliyomo

Vita ya Miaka Saba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Vita vya miaka saba)
Maeneo yote yaliyoathiriwa na Vita ya Miaka Saba      Uingereza, Prussia, Ureno na nchi ndogo      Ufaransa, Hispania, Austria, Urusi, Uswidi, pamoja na koloni na nchi ndogo upande wao

Vita ya Miaka Saba ilitokea kati ya miaka 1756 na 1763. Ilitokana na mashindano ya nchi za Ulaya ikasambaa pande nyingi za dunia. Hivyo imeitwa "Vita Kuu ya Dunia" ya kwanza hata kama jina hilo kwa kawaida linatumiwa kwa ajili ya vita kati ya 1914 na 1918.

Ushirikiano kati ya nchi za Ulaya mwanzoni wa vita ya miaka 7.

Washiriki

[hariri | hariri chanzo]

Washiriki katika vita hii walikuwa nchi za Ulaya na makoloni yao, pia watu wa sehemu mbalimbali za dunia walioshikamana nao.

Walipopigana walikuwa:

Sababu za vita

[hariri | hariri chanzo]

Vita ilianza kwa sababu mbili hasa:

  • ndani ya Amerika ya Kaskazini Ufaransa na Uingereza zilishindana kuhusu upanuzi wa maeneo yao.
  • katika Ulaya Prussia iliwahi kutwaa jimbo la Silesia kutoka Austria na Austria ilitaka kuchukua jimbo hilo tena.
  • nchi nyingi za Ulaya ziliogopa uwezo mkubwa mno wa nchi nyingine ikiruhusiwa kushinda vitani, hivyo ziliamua kuingilia kati.

Mashindano na hofu hizo vilisababisha kutokea kwa makambi hayo mawili makubwa.

Vituo vikuu vya Waingereza (nyekundu) na Wafaransa (buluu) katika Uhindi kabla ya vita

Mapigano

[hariri | hariri chanzo]

Mapigano yalitokea Ulaya hasa Ujerumani, halafu huko Uhindi, Amerika ya Kaskazini, kwenye visiwa vya Karibi, pwani za Afrika na Ufilipino.

Vita ya miaka 7 katika Amerika ya Kaskazini
buluu: eneo la Kifaransa; nyekundu: eneo la Kiingereza kabla ya vita; Ufaransa ilipoteza yote

Matokeo makuu ya vita

[hariri | hariri chanzo]
  • Uingereza ilipata kuwa nchi yenye makoloni mengi zaidi duniani baada ya Hispania ikaelekea kuipiku. Pia ilitawala bahari za dunia kwa kuwa taifa lenye manowari mengi na vituo pamoja na bandari kwenye mabara yote.
  • Uwezo wa Ufaransa ulipunguzwa ikipotewa na makoloni yake katika Amerika ya Kaskazini na kubaki na maeneo madogo tu katika Karibi na Uhindi.
  • Prussia ilitoka vitani kama nchi muhimu ya tano ya Ulaya pamoja na Ufaransa, Austria, Uingereza, na Urusi.

Matokeo ya baadaye

[hariri | hariri chanzo]
  • Msingi wa Kiingereza kuwa lugha ya kwanza duniani uliwekwa kwa sababu kilitumiwa kote katika makoloni ya Uingereza
  • Ushindi wa Uingereza ulikuwa msingi wa mapinduzi na uhuru wa Marekani miaka 13 baadaye. Walowezi walijifunza mitindo ya vita waliposhiriki katika vita upande wa Uingereza na walitumia ujuzi huo baadaye dhidi ya Uingereza. Kuondolewa kwa Ufaransa kulipunguza vizuizi dhidi ya upanuzi wa Marekani katika Amerika ya Kaskazini.
  • Uadui wa Ufaransa dhidi ya Uingereza ulibaki ukaimarishwa na kusababisha usaidizi wa Ufaransa kwa waasi wa Amerika ya Kaskazini mwaka 1776 hadi kuzaliwa kwa taifa jipya la Marekani.
  • Kudhoofishwa kwa Ufaransa kwa sababu ya gharama kubwa ya vita hivyo na ile ya kusaidia Wamarekani baadaye ambayo iliathiri uchumi na sifa za utawala wa kifalme na kuwa sababu muhimu ya mapinduzi ya Kifaransa
  • Ushindi wa Prussia ulisababisha mashindano ya mfululizo kati ya Prussia na Austria juu ya kipaumbele katika Ujerumani yaliyoonekana baadaye hadi vita ya 1866.

Picha za watawala wa nchi shiriki za Vita ya miaka saba

[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vita ya Miaka Saba kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.