Hifadhi ya Virunga
Hifadhi ya Virunga, iliyoita zamani Albert Park, ni Hifadhi ya Taifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliyoundwa mwaka 1925 na hivyo ni hifadhi ya kale kabisa katika Afrika.
Ina utajiri mkubwa wa wanyama na mimea[1]. Kuwepo kwa Okapi kulithibishwa mnamo mwaka 2008. [2].
Hifadhi imeandikishwa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO tangu mwaka 1979. Katika miaka ya hivi karibuni, uwindaji haramu na Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Kongo uliharibia mazingira ya wanyamapori wengi.
Hifadhi inasimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi za Kitaifa za Kongo, Institut Congolais pour la conservation de la Nature (ICCN) na hasa Virunga Foundation, iliyojulikana zamani kama Afrika Conservation Fund (Uingereza).
Historia
[hariri | hariri chanzo]Hifadhi iliundwa mwaka 1925 na Mfalme Albert I wa Ubelgiji kama Hifadhi ya Taifa ya kwanza katika bara la Afrika. Ilianzishwa hasa kulinda masokwe wa milimani wanaoishi katika misitu[3] ya milima Virunga, lakini baadaye ilipanuliwa kaskazini ni pamoja na tambarare za Rwindi, Ziwa Edward na Milima Rwenzori katika kaskazini ya mbali.
Katika miaka 35 ya kwanza, uwindaji haramu ulikuwa mdogo, na matumizi ya rasilimali za Hifadhi kama vile uvuvi na uwindaji kwa wakazi wa eneo yakawa tatizo la kudumu na majaribio yalifanywa kutatua masuala haya.
Wakati Wabelgiji walipoiachia Congo uhuru mwaka 1960 hali mpya imekuja kwa haraka, na hivyo, hifadhi. Ilikuwa ni mwaka 1969 wakati Rais obutu alipoanza kuchukua maslahi binafsi katika hifadhi.
Virunga ilifanya vizuri kwa sehemu bora ya miaka ya 1970. Uwekezaji wa kigeni ulisaidia kuboresha miundombinu na Hifadhi kuwa kituo maalum cha watalii, kupokea kwa wastani wageni 6500 kwa mwaka. Mwaka wa 1979 UNESCO iliteua Hifadhi kama Urithi wa Dunia.[4]
Katikati ya miaka ya 1980 serikali ya Mobutu ilianza kupoteza nguvu na nchi kuingia katika machafuko. Hifadhi iliteswa sana. Ujangili umemaliza mamalia wakubwa wakazi wa Virunga, miundombinu mara kuharibiwa, na askari wengi waliuawa. Mamlaka ya wanyamapori polepole ilipoteza udhibiti wa Virunga na UNESCO kutamka Urithi wa Dunia kuwa "hatarini".[4]
Mwaka 2013 Mfuko wa Wanyamapori Duniani ulipinga mipango ya kampuni ya Uingereza Soco International ya kutafuta mafuta katika hifadhi. [5]Kwa sasa zaidi ya 80% ya Hifadhi ya Virunga zimetengwa kama makubaliano ya mafuta.[6] Ripoti ya Soco International yenyewe ilikiri kwamba kupeleleza mafuta ni uwezekano wa kusababisha uchafuzi wa mazingira usiorekebika na kuleta ujangili kwa hifadhi. Mfuko wa Wanyamapori Duniani ulianzisha kampeni ya kulalamikia Soco [7] ambayo kufikia 30 Agosti 2014 iliacha shughuli zake nchini.
Watendaji wa Mfuko wa Wanyamapori Duniani sasa hukubali kuwa vita juu ya Virunga ni vigumu zaidi. Soco bado haijaachilia uendeshaji na vibali vyake wala kujitoa bila masharti.[8]
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Masokwe wa milimani
-
Bangomba Rwenzori
-
Simba dume wawili wakipumzika karibu na Rwindi
-
Ndovu na nyati
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ (Kifaransa) République démocratique du Congo : Rapport de pays pour la conférence technique internationale de la FAO sur les ressources phytogénétiques (Leipzig; 1996) Ilihifadhiwa 14 Februari 2005 kwenye Wayback Machine.
- ↑ {Rare African okapi seen in wild, tovuti ya BBC ya 11 September 2008
- ↑ Denis, Armand. "On Safari: The story of my life". New York. Dutton, 1963, p. 76.
- ↑ 4.0 4.1 "Virunga National Park - UNESCO World Heritage List". UNESCO World Heritage Centre. UNESCO. Iliwekwa mnamo 22 Januari 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "'Oil threat' to DR Congo's Virunga National Park", BBC Online, BBC News, 31 July 2013. Retrieved on 2 August 2013.
- ↑ "Save Virunga". Save Virunga. Iliwekwa mnamo 2014-04-21.
- ↑ "Keep Oil Exploration Out of Virunga National Park · Causes". Causes.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-04-23. Iliwekwa mnamo 2014-04-21.
- ↑ "Oil Dispute Takes a Page From Congo's Bloody Past". 2014-11-15. Iliwekwa mnamo 2014-11-19.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Virunga National Park travel guide kutoka Wikisafiri
- "Virunga National Park". UNESCO World Heritage Centre. UNESCO. Iliwekwa mnamo 22 Januari 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - BirdLife International. "Important Bird Areas factsheet: Virunga National Park".
- "Visit Virunga National Park".
- "Interview With Emmanuel de Merode, Director of Virunga National Park – National Geographic Blog". blog.nationalgeographic.org. Mei 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Desemba 22, 2017. Iliwekwa mnamo 2017-12-21.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - "Inside the Fight to Save a Dangerous Park", National Geographic Magazine 230 (1), July 2016.
Makala hii kuhusu maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Virunga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |