Nenda kwa yaliyomo

Silvesta Guzzolini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Silvesta alivyochorwa na msanii asiyejulikana katika karne ya 15.
Sanamu yake katika St. Sylvester's College, Kandy, Sri Lanka.

Silvesta Guzzolini (Osimo 1177Fabriano 26 Novemba 1267) alikuwa padri mmonaki wa mkoa wa Marche, Italia aliyerekebisha utawa wa Wabenedikto kwa kuanzisha tawi linaloitwa Wasilvesta.

Papa Klementi IV alimthibitisha kuwa mwenye heri, halafu Papa Klementi VIII alimtangaza mtakatifu mwaka 1598.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Novemba.[1][2]

Mwana wa ukoo maarufu wa Osimo, alitumwa kusoma sheria katika chuo kikuu cha Bologna, halafu Padua.

Lakini alijisikia wito, hivyo akabadili masomo akachukua teolojia na Biblia. Uamuzi huo haukumpendeza baba yake, ambaye kwa sababu hiyo alimfungia nyumbani akikataa kusalimiana naye miaka 10.

Silvesta akawa padri mkanoni huko Osimo akajitosa katika uchungaji kiasi cha kusababisha kijicho cha askofu wake, hasa baada ya kumkosoa kwa mwenendo wake mbaya.[3]

Kisha kutengwa naye, alizidi kutambua ubatili wa ulimwengu alipochungulia kaburi wazi la rafiki yake [4].

Basi, mwaka 1227 alikwenda kuishi upwekeni katika ufukara wa hali ya juu sehemu mbalimbali mpaka alipopewa nafasi nyingine huko Grotta Fucile, karibu na Fabriano, alipoanzisha monasteri.[3]

Huko alifanya toba kali, akila tu majani mabichi na kunywa maji, pamoja na kulala ardhini. Hata hivyo wengi waliamua kumfuata hata ikambidi kuchagua kanuni ya kitawa, ikawa ile ya Benedikto wa Nursia.

Baadaye alijenga monasteri kwenye Montefano, upande wa pili wa eneo la Fabriano, na nyingine 11 sehemu mbalimbali za Italia, hata za kike.[3]

Mwaka 1248 alipewa na Papa Innocent IV, huko Lyon, hati ya uthibitisho kwa shirika lake.

Silvesta alifariki akiwa mkongwe tarehe 26 Novemba 1267.[5]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.