Nenda kwa yaliyomo

Shirika kwa Ukoloni wa Kijerumani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maeneo yaliyodaiwa na shirika la GfdK.
Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Afrika Mashariki 1800-1845
Ukoloni
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Mapambano ya uhuru Tanganyika
Uhuru
Uhuru wa Tanganyika
Mapinduzi ya Zanzibar
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
Samia Suluhu Hassan

Tanzania Portal

Shirika kwa Ukoloni wa Kijerumani (kwa Kijerumani Gesellschaft für Deutsche Kolonisation, GfdK; kwa Kiingereza "Society for German Colonization") lilikuwa shirika la binafsi nchini Ujerumani lililoweka msingi kwa koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani katika eneo la Tanzania ya leo.

Kuundwa na shabaha

[hariri | hariri chanzo]

Shirika lilianzishwa tarehe 28 Machi 1884 na Karl Peters na Wajerumani wengine waliotaka Ujerumani kuingia kati ya mataifa yenye koloni. Shabaha ya shirika ilikuwa kuanzisha makoloni ya Kijerumani katika maeneo nje ya Ujerumani.

Msafara wa Afrika ya Mashariki

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kuundwa kwa shirika tume lake lilisafiri Zanzibar mwaka huohuo wa 1884 kwa shabaha ya kujipatia maeneo kwenye bara la Afrika. Wajumbe wa tume hili walikuwa Karl Peters, Joachim von Pfeil na Karl Jühlke. Kutoka Unguja Peters alivuka bahari akafika Saadani. Kutoka hapa aliendelea sehemu za ndani zaidi alipoanza kufahamiana na machifu katika Useguha, Nguru, Usagara na Ukami aliohamasisha kuweka alama zao kwenye karatasi zenye matini ya kuwa, walikabishi haki zao za kiutawala na kiuchumi kwa shirika. Kuna uhakika ya kwamba machifu wenyewe hawakuelewa maana ya karatasi hizi wala hawakuwa na madaraka yaliyopelekwa kwa shirika la ukoloni.

Hati ya ulinzi na kuundwa kwa Kampuni ya kikoloni

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kurudi Ujerumani mwaka 1885 Peters alitumia "mikataba" hii kwa kupata "hati ya ulinzi" ya serikali ya Ujerumani kwa ajili ya kazi ya shirika katika maeneo husika. Baada ya kupewa hati ya ulinzi Peters aliunda shirika mpya la Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki na kupeleka haki za shirika kuhusu maeneo ya Kiafrika kwake.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]