Nenda kwa yaliyomo

Sherry Palmer

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sherry Palmer
muhusika wa 24

Penny Johnson Jerald kama Sherry Palmer
Imechezwa na Penny Johnson Jerald
Misimu
1, 2, 3
Maelezo

Sherry Palmer ni jina la muhusika wa kipindi cha mfululizo wa televisheni cha Kimarekani cha 24. Uhusika huu ulichezwa na Penny Johnson Jerald. Kiasili ya uhusika huu aliolewa na Seneta wa Maryland na baadaye Rasi wa Marekani Bw. David Palmer. Huyu ni mama mwenye vituko na tamaa zisizo na msingi na baadaye kupelekea kumwingiza matatani.

Pili na tabia zake chafu za ufitinishaji, zilipelekea apewe taraka na mumewe Mh. David Palmer. Ameonekana katika msimu wa kwanza, wa pili, na wa tatu ambamo aliuawa na rafikiye Bi. Julia Milliken, mke wa Alain Milliken aliyeuawa na Sherry kwa kutompa vidonge vyake ya kutuliza maumivu ya moyo wake na kisha baadaye Sherry kakataa kwamba siyo yeye aliyefanya, bali Julia.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]