Chloe O'Brian

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chloe O'Brian
muhusika wa 24
Imechezwa na Mary Lynn Rajskub
Idadi ya sehemu 96
Hali
Yu hai
Misimu
3, 4, 5, 6, 7
Maelezo
Familia Timothy O'Brian
Ndoa Morris O'Brian(Wameachana)
Watoto Prescott O'Brian

Chloe O'Brian ni jina la uhusika wa kipindi cha televisheni cha Kimarekani maarufu kama 24. Uhusika unachezwa na Mary Lynn Rajskub.

Katika uhusika[hariri | hariri chanzo]

Ni mmoja kati ya watu wachache wanaoaminiwa na Jack Bauer, mara nyingi humpa msaada mkubwa hadi ile isiyoruhusiwa. Ameonyesha uwezo wake mkubwa katika matumizi ya kompyuta. Anatumia muda wake mwingi akiwa kwenye vyumba vya kompyuta, ingawa, kuna mara chache alizotumwa aende kwenye uwanja wa mapambano na akalazimika kujifunza namna ya kutumia silaha - hasa kwenye Siku ya 4 na 5. Ukiachia mbali masuala yake binafsi na kijamii, Chloe amepata marafiki kibao CTU na ameonyesha kuwajali na umanifu katika kazi. Huyu ni tegemezi la CTU. Huyu ndiye anayetia utamu katika mfululizo mzima wa 24.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]