Nenda kwa yaliyomo

Ryan Chappelle

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ryan Chappelle
muhusika wa 24

Paul Schulze kama Ryan Chappelle
Imechezwa na Paul Schulze
Misimu
1, 2, 3
Maelezo

Ryan Chappelle ni jina la uhusika wa kipindi cha televisheni cha Kimarekani maarufu kama 24. Uhusika ulichezwa na Paul Schulze. Katika mfululizo huu, Chappelle alikuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Los Angeles katika Kitengo cha Kuzuia Ugaidi (CTU).

Yupo juu ya George Mason na Alberta Green katika kuamuru. Akiwa kama mwikilishi wa kanda, anachukua amri moja kwa moja kutoka kwa Rais. (Ingawa katika Msimu wa 1 alipewa agizo kutoka kwa mmoja wa maofisi wa Pentagon ambalo alilifuata bila kupinga). Mwishoni anaeonekana kuawa na Jack Bauer kwa kufuati agizo lililotolewa na gaidi Stephen Saunders - na wasipofanya hivyo, basi ataachia virusi nchini mwao.

Kwa hili, Jack hakuwa na budi hasa ikiwa hata Rais David Palmer ametoa ruhusa ya kuawa kwa Chappele. Chappele alikuwa kiongozi mzuri kabisa katika CTU. Chappele ni kiongozi pekee aliyekubali maisha yake yapotee kwa ajili ya wananchi. Juu ya hayo, Chappele alikuwa mwoga kimaamuzi - ambavyo huwezi kufananisha na Bill Buchanan.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]