George Mason

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
George Mason
muhusika wa 24
Imechezwa na Xander Berkley
Hali
Amefariki
Misimu
1, 2
Maelezo

George Mason ni jina la uhusika wa kipindi cha televisheni cha Kimarekani maarufu kama 24. Uhusika ulichezwa na Xander Berkley.

Yeye ni Mkurugenzi wa pili wa CTU. Kazi kubwa ilikuwa katika mambo ya utawala, lakini atekwa na Jack Bauer. Mason ndiye anayehusika kwa kukamatwa kwa Bauer na kugundua mwili wa Alan York.

Mason ndiye anayehusika kwa kuongoza msako wa kuiokoa familia ya Bauer na kuzuia njama nzima dhidi ya David Palmer. Mason pia anahusika kwa kukamatwa kwa Nina Myers.

Katika msimu wa 2, Mason dhahiri anajaribu kukimbia katika eneo ambalo linasemekana litafanyiwa uvamizi wa kigaidi, lakini akiwa njiani akapata simu iliyokuwa ikizungumzia kwamba kuna sehemu wanaunganisha mabomu ya nyuklia. Wakati wa mapigano ya risasi, Mason akapiga sehemu iliyokuwa imefunikwa sumu ya hewa.

Hivyo ilimwathiri na akaambiwa atakufa baada ya siku moja toka alipopewa dawa za kupunguza makali. Mason baadaye akaoneka kujitolea mhanga maisha yake kwa kulibeba bomu la nyuklia na kwenda kulipuka nalo kwenye jangwa. Mason pia alikuwa mshabiki wa Jimi Hendrix.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]