Nenda kwa yaliyomo

Msamiati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Msamiati ni orodha ya maneno yote ambayo watu wanajua na wanayatumia, yakiwemo yale magumu

Watu wazima ambao huenda chuo kikuu wanaweza kujua maneno 20,000.

Msamiati wa kusikia na msamiati wa kusoma ni mikubwa kuliko msamiati wa kuzungumza au msamiati wa kuandika, kama watu wanavyoelewa maneno ambayo hawayatumii.

Idadi ya maneno katika lugha ni zaidi ya maneno yaliyotajwa katika kamusi moja. Kamusi moja inaweza kuwa na orodha ya maneno 500,000 (nusu milioni).

Kamusi nyingine inaweza kuwa na maneno mengine ambayo kamusi nyingine haina. Unapoongeza maneno yote katika kamusi hizo, kunakuwa na maneno 750,000 ya Kiingereza. Pia kunaweza kukawa na maneno zaidi ya hayo.

Unaweza kufikiri mwenyewe, "Ikiwa kuna maneno 750,000, tunawezaje kuzungumza na maneno 3000 tu?". Ni kwa sababu, hatuhitaji kujua maneno yote. Unaweza kusema vitu vingi kwa maneno karibu 3,000.

Maneno yaliyotumiwa zaidi ni maneno mafupi. Hiyo ni kweli katika lugha zote.

Msamiati wa lugha hubadilika. Maneno mapya yanazalishwa au maneno yanabadilika maana yake. Maneno kuhusu kompyuta, kama "download" ni mapya kwa lugha ya Kiingereza. Neno jipya la "bling" linatoka katika muziki. Maneno kama "baridi" yametengeneza maana mpya.

Vilevile msamiati tunaweza kusema ni maneno magumu ambayo mtu hayaelewi katika kifungu cha habari fulani. Mfano neno tabasamu: ukimuuliza mtu maana ya neno hilo utapata majibu tofauti.

Ukimtaka mtu atunge sentensi kulingana na neno tajwa unaweza kupata sentensi za aina hii:

Hapa tunaona kuwa neno hili limeelezewa na kila mtu kwa jinsi alivyolizoea katika matumizi, hivyo kwa hapa maana halisi ya neno tutaipata kutokana na lilivyotumika katika sentensi husika.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Msamiati kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.