Matumizi ya lugha ya Kiswahili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Matumizi ya lugha ya Kiswahili ni kama ifuatavyo.

1. Kiswahili hutumika katika kufundishia shule za msingi isipokuwa lugha ya Kiingereza hufundishwa kama somo.

2. Kiswahili hutumika katika vyombo vya habari, mfano redio na runinga.

3. Kiswahili hutumika katika nyanja mbalimbali za kiserikali, mfano Mahakama ya mwanzo na ya kati.

4. Pia Kiswahili hutumika kama somo katika shule za sekondari hadi chuo kikuu.

5. Kiswahili hutumika katika shughuli za michezo mbalimbali.

6. Kiswahili hutumika katika nyumba za ibada kutolea mawaidha na mahubiri, mfano kanisani na msikitini.

7. Pia Kiswahili hutumika katika shughuli za kibiashara kama lugha ya mawasiliano miongoni mwa watu.

8. Kiswahili hutumika katika shughuli za kiofisi.