Michael Scofield

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uhusika wa Prison Break

Michael Scofield
Mwonekano wa kwanza: Pilot
Msimu: 1,2,3,4
Imechezwa na: Wentworth Miller
Dylan Minnette (Michael Scofield mdogo)
Pia anajulikana kama: Fish
Snowflake
Pretty
Phineas McClintock
Wayne Merrick
Michael Crane
Superstar
Waterboy
Engineer
Officer Mathers
Familia: Aldo Burrows (baba) (amekufa)
Christina Rose Scofield (mama) (amekufa)
Lincoln Burrows (kaka)
LJ Burrows (mtoto wa kaka yake)
Mahusiano: Nika Volek (mke wa uongo)
Sara Tancredi (kipenzi cha roho)
Veronica Donovan (rafiki wa familia)(amekufa)

Michael Scofield ni jina la mhusika mkuu wa tamthilia ya Kimarekani ya Prison Break. Uhusika huu ulichezwa na Wentworth Miller. Mhusika huyu humu kacheza kama ana umri wa miaka 31. Mhusika huyu anaanza kuonekana akiwa kama mtu aliyejaribu kuiibia benki ili aweze kutupwa jela ambapo kaka yake, Lincoln Burrows (Dominic Purcell), ameshikiliwa hadi hapo hukumu yake ya kifo itakapofika.

Kigezo cha mfululizo huu wa Prison Break, una husisha ndugu wawili na Michael ana fanya mpango wa kusaidia kumtorosha Lincoln kutoka kwenye hukumu yake ya kifo. Ikiwa kama sheria za uhusika mkuu, Michael amepata kucheza katika kila sehemu ya mfululizo huu mzima.

Ingawa wote Lincoln na Michael ndiyo wahusika wakuu wa mfululizo huu, lakini Michael amecheza katika sehemu nyingi sana kuliko Lincoln, ususani katika msimu wa kwanza na watatu.

Katika mfululizo, pia kunaonyeshwa mahusiano ya awali kati ya Michael na ndugu yake, na sababu zilizopelekea Michael kufikiria kumsaidia Lincoln kutoroka jela dhidi ya hukumu ya kifo. Katika sehemu za awali, yaani picha inayomwonyesha Michael akiwa mdogo, zaidi ilichezwa na Dylan Minette.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]