Gretchen Morgan
Mandhari

Uhusika wa Prison Break | |
---|---|
Gretchen Morgan | |
Mwonekano wa kwanza: | Orientación |
Msimu: | 3,4 |
Imechezwa na: | Jodi Lyn O'Keefe |
Kazi yake: | Askari wa jeshi wa zamani wa US Kachero wa The Company |
Familia: | Rita Morgan (Dada yake) Emily Morgan (Binti yake) |
Gretchen Louise Morgan (amezaliwa tar. 29 Machi 1977 mjini Johnstown, West Virginia) ni jina la kutaja uhusika wa katika kipindi cha televisheni cha Prison Break. Uhusika huu umechezwa na Jodi Lyn O'Keefe. Mhusika huyu alianza kuwa kama mmoja kati ya wahusika wakuu wa mfululizo huu baada ya kufikia katika msimu wa tatu wa mfululizo huu.
Huyu ni mwanadada asiye na huruma, hana subira, na asiye sita kumchinja mtu aliyejaribu kukwaza mpango wake usifane. Huyu mwanamke aliyeshika nafasi ya aliyekuwa adui mkuu wa Msimu wa 2 wa mfululizo huu, Bw. William Kim, ameonekana kuwa na uwezo mkubwa wa utesaji na kusimama vilivyo katika swala zima la martial arts.