Nenda kwa yaliyomo

Maricruz Delgado

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Camille Guaty ni muhusika aliye tumia jina la Maricruz Delgado katika kipindi cha mfululizo wa televisheni cha Kimarekani cha Prison Break
Uhusika wa Prison Break
Maricruz Delgado
Mwonekano wa kwanza: Pilot
Msimu: 1,2,3,4
Imechezwa na: Camille Guaty

Maricruz Delgado ni jina la mhusika katika kipindi cha mfululizo wa televisheni cha Kimarekani cha Prison Break. Uhusika ulichezwa na Camille Guaty. Mhusika huyu alicheza kama mwanamke wa Fernando Sucre. Alikutana na Sucre miaka mitatu nyuma kama jinsi inavyojieleza katika sehemu ya pilot, na akaendelea kuwa naye hadi hapo alipokuja kutiwa kizuizini.

Akiwa jela, Sucre alimwomba Maricruz amsubirie hadi apo atakaporudi kisha wafunge ndoa na mama huyo alikubali. Maricruz baadaye akajijua kama ni mjamzito (ya Sucre). Tendo la Maricruz kuwa na mimba, Sucre alizidi kupata mzuka wa kutaka kutoroaka jela.

Furaha yake ya kuwa baba haikudumu sana baada ya kugundua kuwa Hector ana mahusiano na Maricruz, hivyo Maricruz hatomtembelea Sucre kwa kufuatia mahusiano mpya yake mpya na Hector.

Hilo ndilo lilizidi kumfanya Sucre kuongeza juhudi zake za kutaka kutoroka. Maricruz akavishwa pete na Hector na kisha wakasafiri zao na kuelekea mjini Las Vegas kwenda kufungua ndoa, na kusabishia Sucre kujaribu kuzuiya harusi hiyo.

Baadaye, ilikuja kugundulika kwamba Maricruz amempiga chini Hector kwenye kilele cha ndoa, kitendo ambacho kilimtia mtawasha Sucre kumfuatilia mama mtoto wake. Wawili hao walikuja kuungana tena kunako uwanja wa ndege wa mjini Ixtapa, Mexiko na kuwenda kukaa katika nyumba ya shangazi yake Sucre.