Nenda kwa yaliyomo

Brad Bellick

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uhusika wa Prison Break

Brad Bellick
Mwonekano wa kwanza: Pilot
Msimu: 1,2,3,4
Imechezwa na: Wade Williams
Pia anajulikana kama: Boss; Captain; Brad; Brian; Cap'n;
Kazi yake: Captain wa Fox River
Ofisa wa mapolisi jela (Msimu wa 1)
Mshauri wa FBI (Msimu wa 2)
Familia: Edna Bellick (Mama)

Bradley "Brad" Bellick lilikuwa jina la kutaja uhusika wa katika tamthiliya ya Kimarekani ya Prison Break. Uhusika huu ulichezwa na Wade Williams. Akiwa kama mmoja kati ya kiongozi wa mfululizo huu wa Prison Break, ameshiriki katika misimu yote minne ya mfululizo.

Uhusika ulitambulishwa ukiwa kama Captain Brad Bellick, akiwa kama kiongozi wa maofisa wa polisi wa jela ya Fox River State Penitentiary. Kiasili, alikuwa adui mkubwa wa Michael Scofield na kikosi kizimu cha waliotoroka jela. Katika msimu wa pili, uhusika ulibadilika kabisa kutoka kule jela, ambampo ilimwezesha kuwa mmoja kati ya wahusika wakuu wa mfululizo huu.

Akiwa yeye sio mwenye akili nyingi kama jinsi alivyo Scofield au Agent Mahone, amepata kujionyesha kuwa na yeye kuwa mjanja wa hali ya juu, na katika mfululizo wa pili aliweza kuwakamata watorkaji kadhaa waliotorka kule Fox River na kusafiri hapa na pale katika Amerika kwa kutumia bajeti ndogo kabisa.

Katika mfululizo wa nne, Bellick amekuwa mmoja kati ya wanachama wa Scofield waliojitolea kuitafuta Scylla, lakini alijitolea mhanga maisha yake kwa dhumuni la kuulinda mpango wao.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]