Nenda kwa yaliyomo

Alexander Mahone

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uhusika wa Prison Break

Kachero Alex Mahone
Alexander Mahone
Mwonekano wa kwanza: Manhunt
Msimu: 2,3,4
Imechezwa na: William Fichtner
Pia anajulikana kama: Alex
Familia: Pam Mahone (mke wake wa zamani)
Cameron (mtoto wake, amefariki)
Mahusiano: Kacee Franklin (mke wake)

Alexander Mahone ni jina la kutaja uhusika wa katika kipindi cha televisheni cha Kimarekani cha Prison Break. Uhusika huu ulichezwa na William Fichtner. Uhusika huu ulitambulishwa katika sehemu ya pili ya msimu wa mfululizo huu. Amecheza katika sehemu maarufu za mwanzoni kabisa na tangu hapo akawa anaonekana katika kila sehemu ya mfululizo huu.

Mahone alikuwa Kachero Maalum wa FBI, alibobea katika fani ya kuwawinda wafungwa waliotoroka, na ana uzoefu huo kwa takriban miaka kumi na minne.[1] Baada ya nyota wa mfululizo huu, Michael Scofield (imechezwa na Wentworth Miller), kufaulu kuwatorosha wafungwa wenzake kutoka katika jela ya Fox River State Penitentiary, Mahone amesaini mkataba na kukusanya nguvu ili kuwarudisha watoro wote waliotoroka. Humu kacheza kama ana umri wa miaka 42.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Otis", Prison Break season 2 episode 2.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]