Nenda kwa yaliyomo

Wentworth Miller

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wentworth Miller

Wentworth mnamo Septemba 2011
Amezaliwa 2 Juni 1972 (1972-06-02) (umri 53)
Chipping Norton, Oxfordshire, Uingereza
Miaka ya kazi 1998–hadi leo

Wentworth Earl Miller III (amezaliwa tar. 2 Juni 1972) ni mwigizaji wa filamu wa Kimarekani-Kiingereza, aliyetunukiwa tuzo ya Golden Globe akiwa kama mwigizaji bora wa filamu na tamthiliya. Amejizolea umaarufu mkubwa baada ya kucheza kama Michael Scofield kutoka katika tamthilia ya Prison Break iliyokuwa inarushwa hewani na televisheni ya FOX Network.

Maisha yake na wasifu

[hariri | hariri chanzo]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Miller alizaliwa Chipping Norton, Oxfordshire, Uingereza, ambapo baba yake alikuwa akiishi huku akisoma katika chuo cha Oxford. Familia yake baadae ilihamia Park Slope, Brooklyn, New York, kipindi ana mwaka mmoja. Ana madada wawili, Leigh na Gillian. Alipata elimu yake pale Midwood High School iliyopo Brooklyn, New York USA. Alihitimu masomo yake katika Chuo cha Princeton akiwa na shahada ya Fasihi ya Kiingereza.

Katika mahojiano, Miller alibainisha kuwa asili yake ni mchanganyiko. Akimaanisha kuwa baba yake ni Mmarekani-Mwafrika, Muingereza, Muitalia, Mjerumani na nusu Mcherokee[1] na mama yake ni Mrusi, Mfaransa, Mdachi na Msyria.

Maisha ya Uigizaji

[hariri | hariri chanzo]

Miller kwa mara ya kwanza aliigiza nafasi ya nyota kama David katika tamthilia fupi Dinotopia ya ABC. Baada ya kuonekana katika maigizo tofauti tofauti ya kwenye runinga, alihamia kwenye filamu ya mwaka 2003 The Human Stain akicheza nafasi ya nyota msaidizi. Aliigiza kama Anthony Hopkins kijana. Miller alianza kuonekana kwenye runinga kwenye tamthilia ya Buffy the Vampire Slayer (Go Fish 1998).

Mwaka 2005, Miller alicheza kama Michael Scofield kwenye tamthilia ya Prison Break ya FOX Network. Amigiza kama kaka anayemjali nduguye kwa kuandaa na kufanikisha mpango mzima wa kumtorosha jela kaka yake Lincoln Burrows ili kumuepusha na adhabu ya kifo aliyohukumiwa kimakosa. Umahiri aliouonyesha kwenye tamthilia hiyo ulipelekea kujipatia tuzo ya Golden Globe 2005 kwa kuchaguliwa kuwa Muigizaji Bora wa Kiume Kwenye Tamthilia.[2] Miller ameonekana kwenye video mbili za muziki za mwanadada Mariah Carey na alipata mchango mkubwa kutoka kwa Carey kutokana na video ya nyimbo We Belong Together. Miller anadai kuwa umahiri wa video hiyo umechangia kwa kiasi kikubwa kuwashawishi waandaaji kumpa nafasi ya nyota kwenye tamthilia iliyojizolea umaarufu ya Prison Break. Anasema, "Mariah ni maarufu kimataifa. Siku mbili nilizokuwa naigiza kwenye video zake zimenisaidia sana kisanaa, zimenitangaza zaidi kuliko jambo lolote nililowahi kulifanaya kabla ya Prison Break. Ninashukuru sana kwa nafasi ile."

MwakaJinaKamaMaelezo
Tamthilia
1998Buffy the Vampire SlayerGage Petronzi
  • Season 2, episode 20: "Go Fish"
2000ERMike Palmieri
  • Season 7, episode 1: "Homecoming"
2000Time of Your LifeNelson
  • Season 1, Episode 6: "The Time the Truth Was Told"
  • Season 1, Episode 11: "The Time They Got E-Rotic"
2002DinotopiaDavid ScottTamthilia fupi
2005Ghost WhispererSgt. Paul Adams
  • Season 1, episode 1: pilot
2005Joan of ArcadiaRyan Hunter
  • Season 2, episode 21: "Common Thread"
  • Season 2, episode 22: "Something Wicked This Way Comes"
2005–SasaPrison BreakMichael ScofieldTamthilia
Filamu
2001Room 302Server #1Filamu fupi
2003UnderworldDr. Adam Lockwood
2003The Human StainColeman Silk mdogo
2005Stealthvoice of EDI
2005The ConfessionsPrisonerShort film
Video za Miziki
2005"It's like That"Mysterious love interestVideo ya Muziki ya Mariah Carey
2005"We Belong Together"Mysterious love interestVideo ya Muziki ya Mariah Carey
  1. Christopher Loudon, "Wentworth Miller's Big Break", Sir. Canada's International Magazine of Style for Him, Spring 2006, p. 61.
  2. "2006 Golden Globe Nominations & Winners". Hollywood Foreign Press Association. Januari 26 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-02-17. Iliwekwa mnamo 2007 02 26. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= na |date= (help)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]