Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Michael Scofield

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Michael Scofield ni jina la mhusika mkuu wa tamthilia ya Kimarekani ya Prison Break. Uhusika huu ulichezwa na WentworthMiller . Mhusika huyu humu kacheza kama ana umri wa miaka 31. Mhusika huyu anaanza kuonekana akiwa kama mtu aliyejaribu kuiibia benki ili aweze kutupwa jela ambapo kaka yake,

(Dominic Purcell), ameshikiliwa hadi hapo hukumu yake ya kifo itakapofika.

Kigezo cha mfululizo huu wa Prison Break, una husisha ndugu wawili na Michael ana fanya mpango wa kusaidia kumtorosha Lincoln kutoka kwenye hukumu yake ya kifo. Ikiwa kama sheria za uhusika mkuu, Michael amepata kucheza katika kila sehemu ya mfululizo huu mzima.

Ingawa wote Lincoln na Michael ndiyo wahusika wakuu wa mfululizo huu, lakini Michael amecheza katika sehemu nyingi sana kuliko Lincoln, ususani katika msimu wa kwanza na watatu.

Katika mfululizo, pia kunaonyeshwa mahusiano ya awali kati ya Michael na ndugu yake, na sababu zilizopelekea Michael kufikiria kumsaidia Lincoln kutoroka jela dhidi ya hukumu ya kifo. Katika sehemu za awali, yaani picha inayomwonyesha Michael akiwa mdogo, zaidi ilichezwa na Dylan Minette.

Jamii: Wahusika wa Prison Break

Start a discussion about Michael Scofield

Start a discussion