Mahamadou Diarra
Mahamadou Diarra (alizaliwa Bamako, Mali, 18 Mei 1981)[1] ni mchezaji wa kiungo wa kandanda.
Yeye ana uzito wa kilo 82 (paundi 181) na urefu wa mita 1.82 (futi za miguu 6). Yeye alikuwa maarufu alipocheza na timu ya taifa ya Mali ambako alikuwa nahodha wa timu. Diarra alianza kazi yake ya kandanda katika OFI, klabu ya kandanda katika kisiwa cha Krete. Alikuwa na umri wa miaka 17. Mwaka 2002, Diarra aliichezea klabu ya Kifaransa, FC Lyon. Kwa Lyon kwa miaka minne, alikuwa mchezaji aliyeanzisha mpira.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2006, Manchester United na Real Madrid walimtaka kwenye timu yao. Aliingia na Real Madrid kama mchezaji wa jezi namba 6, jezi ya zamani ya Iván Helguera, na walimlipa fehda za kiuropa kiasi cha yuro milioni 26 (€26 million). Wakati wa msimu wake wa kwanza, alicheza michezo 33 kati ya michezo 38, kama sehemu ya timu ya wanaume wawili pamoja na José Antonio Reyes. Wakati wa msimu wa pili, Madrid ilikuwa na kocha mkuu mpya, Bernd Schuster. Diarra alikuwa chaguo la kwanza kiungo wa kujihami wa Schuster.
Mwaka 2008 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, Diarra aliumiza goti lake. Alirudi kucheza tena haraka sana na alihitaji upasuaji mnamo Novemba ambapo alilazimika kuweka kando mapumziko ya msimu. Mwaka 2011, Diarra aliondoka Real Madrid na alianza kucheza kwa mwaka mmoja katika AS Monaco.
Aliingia na Fulham F.C., ambako Ligi Kuu ya Uingereza, mwaka 2012.[2] Fulham alipumzika kwa msimu wa 2012-13, ila alijiunga tena mwisho wa msimu wa 2013-14. Kwa msimu wa 2016-17, alicheza katika ngazi ya pili ya Uingereza. Alimaliza kazi yake pamoja na Fulham FC mwezi wa kwanza mwaka 2015.
Ana jumla ya michezo 431 na magoli 29 katika kazi yake na alishinda ligi ya michuano kwa misimu sita mfululizo. Wakati wa kucheza katika Lyon, yeye hucheza mara nyingi pamoja na Michael Essien. Amekuwa mmoja wa kiungo bora zaidi cha kujihami cha Ulaya, kama Claude Makélélé na Patrick Vieira.
Katika FC Lyon, alishinda Trophée des Champions: miaka 2003, 2005, na 2006. Alishinda pia Ligue 1 ya UEFA: misimu ya 2002-03, 2003-04, 2004-05, na 2005-06. Katika Real Madrid, alishinda La Liga: misimu ya 2006-07 na 2007-08. Alishinda pia Supercopa de España mwaka 2008.[3]
Nguvu na Udhaifu
[hariri | hariri chanzo]Nguvu zake kuu ni nguvu zake katika hewa na kiwango cha kazi (Kiwango cha kazi ni kiasi cha muda katika mchezo kwamba mchezaji anachangia kukimbia na kushinikiza wakati hawana mpira.) ila udhaifu wake ni hasira yake.
Maisha Binafsi
[hariri | hariri chanzo]Mahamadou Diarra ni Mwislamu. Alipoishi Ulaya, hakuwa na shida pamoja na makocha wake na dini yake. Hazungumzii sana maisha yake binafsi. Katika Instagram na Twitter, chapisho lake la mwisho lilikuwa mwaka 2017.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Mahamadou Diarra", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-06-25, iliwekwa mnamo 2019-07-25
- ↑ S. Gordon. "EPL: Mahamadou Diarra Signs for Fulham". Bleacher Report (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-07-25.
- ↑ "Mahamadou Diarra - Player Profile". www.transfermarkt.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-07-25.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mahamadou Diarra kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |