Instagram

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Instagram ni mtandao wa kijamii unaoruhusu mtumiaji kupata huduma ya kushirikisha picha za kawaida na za video mtandaoni.

Programu hii hutumika katika simu aidha za iPhone au mfumo uendeshaji wa Android. Programu inakupa fursa ya kuchukua picha na video, na kuzipitisha katika vichujio vyake ili itakate na kisha kuishirikisha na wale wanaokufuata. Vilevile inakupa fursa ya kushirikisha na mitandao mingine ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, JamiiTalk, Tumblr na Flickr.[1]

Mtandao huo uliundwa na Kevin Systrom na Mike Krieger na kutolewa rasmi tarehe 6 Oktoba 2010. Hivi sasa unamilikiwa na kampuni ya Facebook baada ya kununuliwa kwa dola za Kimarekani bilioni 1 Aprili 2012.

Baada ya kuanzishwa mwaka 2010, Instagram ilipata umaarufu mkubwa na kupata watumiaji milioni moja ndani ya miezi miwili, milioni 10 ndani ya mwaka mmoja na milioni 800 hadi Septemba 2017. Hadi Oktoba 2015 kulikuwa na picha bilioni 40 toka kwa watumiaji.

Historia

Kevin Systrom aliweka picha ya kwanza kwenye mtandao huo tarehe 16 Julai 2010. [2][3] The photo shows a dog in Mexico and Systrom's girlfriend's foot; the photo has been enhanced using Instagram's X-PRO2 filter.[4]

Tarehe 6 Oktoba 2010 app rasmi ya kwanza ya Instagram ilitolewa.[5][6]

Matangazo

Kama ilivyo kwa mitandao mingine ya kijamii, Instagram inapata mamilioni ya fedha toka kwenye matangazo. Mnamo Oktoba 2013, Instagram ilianza jitihada za kupata fedha kupitia matangazo ya video na picha nchini Marekani. [7][8] Mnamo Juni 2014, Instagram ilitangaza ujio wa matangazo nchini Uingereza, Canada na Australia.[9]

Mnamo Mei 2016, Instagram ilitangaza uzinduzi wa zana mpya za akaunti za biashara, ikiwa ni pamoja na maelezo mafupi ya biashara, na uwezo wa kugeuza picha, video au maandishi kuwa matangazo moja kwa moja kutoka kwenye programu ya Instagram yenyewe.[10]

Mnamo Februari 2016, Instagram ilitangaza kwamba ilikuwa na matangazo 200,000.[11] Hii iliongezeka hadi kwa watangazaji wa kazi 500,000 mwezi Septemba 2016,[12] na milioni moja mwezi Machi 2017.[13]. Programu mbalimbali zimejitokeza kuwezesha watangazaji kujitanza kwenye Instagram kutokana na umaarufu wake.

Kutumia Instagram

Unapotumia programu ya Instagram, yafaa kwanza uangalie ni heshitegi gani ambazo zinapendwa sana na watu na ambazo zina wafuasi wengi. Ni vizuri pia uwe na picha maalumu ambayo inaonyesha wewe ni nani na taarifa ndogo kukuhusu ili wafuasi wako waweze kujua msimamo wako na masuala unayozingatia.

Ili kupata wafuasi wengi, inabidi uwe ukijipiga picha nyingi mara kwa mara na kuziweka katika mtandao. Picha zenyewe zafaa ziwe zimepigwa vizuri na kamera au simu ili ziwe wazi na kuonekana kwa urahisi. Waweza pia kujua jinsi unavyoendelea katika kupata wafuasi na picha zako kupendeka kwa kufanya ukaguzi ili ujue kama waendelea vizuri na masuala yako yanafuatiliwa na watu.

Instagram pia inakupa nafasi ya kutoa hadithi yako kwa Instagram stories.

Marejeo

  1. Frommer, Dan (November 1, 2010). Here's How To Use Instagram. Business Insider. Iliwekwa mnamo May 20, 2011.
  2. Instagram post by Kevin Systrom • Jul 16, 2010 at 9:24pm UTC.
  3. Here's The First Instagram Photo Ever.
  4. This is Instagram's first photo ever.
  5. Siegler, MG (October 6, 2010). Instagram Launches with the Hope of Igniting Communication Through Images. AOL. Iliwekwa mnamo April 8, 2017.
  6. Welcome to Instagram. Instagram (October 5, 2010). Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-08-25. Iliwekwa mnamo April 8, 2017.
  7. Panzarino, Matthew (October 3, 2013). Instagram To Start Showing In-Feed Video And Image Ads To US Users. AOL. Iliwekwa mnamo April 23, 2017.
  8. Covert, Adrian (October 3, 2013). Instagram: Now with ads. CNN. Iliwekwa mnamo April 23, 2017.
  9. Dove, Jackie (June 9, 2014). Instagram will introduce ads in the UK, Canada and Australia 'later this year'. Iliwekwa mnamo April 23, 2017.
  10. Perez, Sarah (May 31, 2016). Instagram officially announces its new business tools. AOL. Iliwekwa mnamo April 23, 2017.
  11. Ha, Anthony (February 24, 2016). There Are Now 200K Advertisers on Instagram. AOL. Iliwekwa mnamo April 23, 2017.
  12. Ha, Anthony (September 22, 2016). And now there are 500K active advertisers on Instagram. AOL. Iliwekwa mnamo April 23, 2017.
  13. Ingram, David (March 22, 2017). Instagram says advertising base tops one million businesses. Thomson Reuters. Iliwekwa mnamo April 23, 2017.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Instagram kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.