Mtandao wa kijamii

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mtandao wa kijamii au Mitandao ya kijamii ni wavuti au huduma ambapo watu huongea , au hujumuishwa pamoja na watu wengine aidha ndani ya nchi au ulimwenguni. Huduma ya Mitandao ya Kijamii inaweza kuunganisha watu wenye shauku/mapenzi ya aina moja (kama vile mpira wa miguu, shule, ndondi, vyakula aina mbalimbali, filamu, dini na kadhalika) pamoja na urafiki. Sehemu kubwa ya mitandao ya kijamii inakupa fursa ya kutengeneza taarifa zako katika ukurasa wako ikiwa ni pamoja na picha na maelezo kiasi kuhusu wewe mwenyewe. Hasa yale ya msingi, unaishi wapi, una asili ya wapi, elimu, nini unapenda na kadhalika.

Mitandao ya kijamii ilianza kupendekeza tangu hatua za awali za uvumbuzi wa wavu wa walimwengu kwenye mwaka 1993.[1] Baadhi ya mitandao ya kijamii ambayo ni maarufu sana ni pamoja na Facebook na Twitter inasaidia kuongeza kasi ya mawasiliano ulimwenguni. Hata matumizi ya simu za mkononi zimeanza kupungua umaarufu wake hasa kwa mtindo wa uharaka wake wa kupeana jumbe kupitia mitandao hii.

Mitandao ya kijamii inatumika kuwaleta watu pamoja na kujenga urafiki miongoni mwao. Mitandao ya kijamii inatumika kupeana taarifa na watu wengine. Mitandao mingi ya kijamii inapatikana katika simu za mikononi hasa zile simujanja. Kuna baadhi ya makampuni yanafungia uwezo wa kuingia katika mitandao ya kijamii hasa kwa malalamiko ya kwamba waajiriwa wanapoteza muda mwingi katika mitandao hiyo.

Oroha ya mitandao ya kijamii[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. The Network Nation 2 by S. Roxanne Hiltz and Murray Turoff (Addison-Wesley, 1978, 1993)