Nenda kwa yaliyomo

Simu za mikononi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Simu za mkononi)
Siemens AX72
Nokia 3310
Ndani ya simu za mkononi.

Simu ya mkononi (lakabu simu ya kiganjani, simu bila waya, simu-mnara, simu-selula, rununu, rukono[1]) ni simu ndogo inayobebeka.

Simu ya mkononi inaweza kutumika kwa mawasiliano ya mbali bila waya. Inafanya kazi kwa kuwasiliana na kituo cha mawasiliano kwa njia ya mnara (vilevile huita "mnarani") ambayo inaunganisha na mtandao mkuu wa simu. Ikiwa inatembea, kama simu inakuwa mbali sana na mnara iliyoungana nao awali, ule mnara unatuma ujumbe kwa mnara mwingine wa karibu kupokea mawasiliano. Utaratibu huu unasaidia simu isikatike, hivyo basi mawasiliano yanaendelea kwa kuunganishwa huko. Kupasiana huko kwa minara (lugha ya kitaalamu "hand-off"), kunatokea kiasi kwamba hata mtumiaji hawezi kujua kitu kama hicho kimetokea.

Teknolojia hii wakati ilipoanza ilikuwa ghali mno. Lakini kadiri inavyozidi kujulikana kutumika, ndivyo inavyozidi kuwa na gharama za chini, kiasi kwamba siku hizi karibu kila mtu anaweza kumudu gharama za matumizi ya simu ya mkononi.

Muundo mpya wa simu za mkononi unaitwa "simu janja" au "simu mtelezo". Muundo huu umekuwa maarufu ndani ya muda mfupi. Sehemu kubwa ya simu zilizotengenezwa kuanzia mwaka wa 2010 ni "simujanja". Zinaweza kutumika kama tarakilishi na vilevile kupiga simu.

  1. Ulyseas, Mark (2008-01-18). "Of Cigarettes And Cellphones". The Bali Times. Iliwekwa mnamo 2008-02-24.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.