Nenda kwa yaliyomo

Wavuti wa Walimwengu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya WWW jinsi ilivyopangwa katika mazingira ya wikipedia ya Kiingereza

Wavuti wa Walimwengu (kifupi: WWW; pia: Wavuti; Kiingereza: World Wide Web), ni sehemu ya tovuti yenye wavuti nyingi. Sehemu nyingine za tovuti, kama huduma ya baruapepe (email) si sehemu ya WWW.

Tovuti za WWW zinafanywa na kurasa zenye matinikivo (hypertext) zinazoelekezana kwa njia ya viungokivo (hyperlinks). Yaliyomo ya wavuti hizo ni mara nyingi matini (text) pamoja na picha za mgando na za video, hati za sauti au muziki.

Kati ya lugha za mantikikivo zinazotumiwa zaidi ni HTML.

Chanzo[hariri | hariri chanzo]

WWW ulianzishwa mwaka 1989 na Tim Berners-Lee kwenye taasisi ya CERN huko Geneva, Uswisi. Alitunga namna mpya ya ukurasa kwa kutumia lugha ya HTML. Alilenga kupata nafasi ya kubadilishana matokeo ya kazi yake na wataalamu wengine. Kwa maneno yake mwenyewe:

“The WorldWideWeb (W3) is a wide-area hypermedia information retrieval initiative aiming to give universal access to a large universe of documents.”
"Wavuti wa Walimwengu ni mradi wa upatikanaji wa habari kutoka eneo kubwa kwa njia ya hypermedia kwa shababa ya kurahisisha njia za kufikia idadi kubwa ya hati."
(Tim Berners-Lee)

Jina[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Machi 1989 Berners-Lee alitumia kwa mradi wake jina la "Mesh" lililofutwa tena kwa sababu lilikuwa karibu mno na neno "mess" (=fujo). Baadaye alijaribu kutumia majina ya "Mine of Information" (ing. "Mgodi wa habari") au "The Information Mine" lakini vifupi vyao "MOI" (kwa Kifaransa "mimi") na TIM (jina lake mewenyewe) yalikuwa na harufu ya ubinafsi. Pia picha ya "mgodi" ilionekana haifai maana mgodi ni mahali pa kuchukulia kitu lakini wavuti ni pia mahali pa kupelekea habari, si kujipatia pekee. [1]

Hatimaye Berners-Lee alibuni majina ya "Web" ("utando") na "World Wide Web". Jina la "web" lilionekana kufaa vema kutokana na matumizi ya jina katika hisabati kwa wavu wa vinundu ambako kila kimoja kimeunganishwa na kingine.[2]

Mfumo wa wavuti[hariri | hariri chanzo]

Berners Lee alibuni misingi mitatu kwa kuanzisha wawuti wa walimwengu:

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Pendekezo la Berners-Lee kwa uongozi wa CERN la mwaka 1989
  2. WorldWideWeb: Proposal for a HyperText Project (1990)