Nenda kwa yaliyomo

HTML

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

HTML ni kifupi cha "HyperText Markup Language" au Lugha ya kutunga matini ya mtandao. Ni aina ya lugha ya matinikivo (hypertext) inayotumiwa ili wavuti uonekane mtandaoni jinsi inavyotakiwa. HTML ni lugha ya matinikivo inayotumiwa zaidi kwenye wavuti wa walimwengu (WWW).

Ni mchanganyiko wa lugha ya kawaida na misimbo ya pekee inayoieleza tarakilishi kuonyesha maandishi, picha au rangi kwa namna fulani jinsi inavyotakiwa.

Programu ya kivinjari (au kisakuzi - "browser") kama Firefox au Internet Explorer inasoma lugha hii ya HTML inapoambiwa jinsi gani kuonyesha ukurasa. Ukurasa wa wavuti unaweza kuonyesha maandishi, viungo, picha au hata sauti na video.

HTML hutumia amri za pekee zinazoitwa msimbo ("tag"). Misimbo hii hutokea mara nyingi kwa jozi: msimbo funguzi unaambia kivinjari kuanza kazi fulani, na msimbo funga unasema kazi hii inakwisha.

Kuna misimbo mingi tofauti na kila mmoja una kazi yake maalumu.

Misimbo funguzi huwa na neno la kuamrisha ndani ya vibano pembe. Kwa mfano "title" ni amri ya kuonesha maneno kama kichwa. Sasa ili yaonekane kama amri hufungwa ndani ya vibano pembe <title>; sasa programu inajua kuionyesha kama kichwa. Mwisho wa kichwa unaelezwa kwa msimbo </title>.

Yafuatayo ni mfano wa ukurasa wa HTML:

<!doctype html>
<html>
  <head>
    <meta charset="UTF-8">
    <title>Hiki ni kichwa cha ukurasa</title>
  </head>
  <body>
    <p>Hii ni ibara ndani ya maandishi</p>
  </body>
</html>

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]