Android

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Android robot.svg

Android ni jina la aina ya mfumo huria wa uendeshaji wa simu za mikononi. Mfumo huu hutumiwa hasa katika simujanja, kama vile Google inavyomiliki Google Nexus, vilevile kampuni nyingine zinafanya hivyo hivyo ikiwa ni pamoja na HTC na Samsung. Mfumo huu wa uendeshaji umepata kutumika pia katika tablet kama vile Motorola, Xoom na Amazon Kindle Fire. [1]

Google wanasema zaidi ya simujanja milioni 1.3 zenye mfumo wa Android zinauzwa kila siku.[2] Hii imeifanya Android kuwa miongoni mwa mfumo wa uendeshaji wa simu unaotumika sana duniani.

Programu za Android[hariri | hariri chanzo]

Programu za Android, zinaitwa "apps", ambazo zinatoka Duka la Google Play Store. Programu hizi zinatumia mtindo wa .apk. Programu za Android zimetengenezwa na Python, C, C++, au lugha za Java programming lakini Kusano za mtumiaji daima hutengenezwa kwa kutumia Java na XML. Kuna apps zaidi ya milioni 2.8 zinapatikana katika Android.[3]

Matoleo ya Android na majina yake[hariri | hariri chanzo]

Samsung Galaxy yenye toleo la Android

Kila toleo la bidhaa la Android lina namba na jina linatokana na majina ya vitu vitamutamu. Namba za matoleo na majina yake ni:

 • Matoleo ya Beta: Ni Astro na Bender
 • 1.5: Cupcake
 • 1.6: Donut
 • 2.0 and 2.1: Eclair
 • 2.2: Froyo (FROzen YOgurt)
 • 2.3: Gingerbread
 • 3.x: Honeycomb (a tablet-only version)
 • 4.0: Ice Cream Sandwich
 • 4.1, 4.2 and 4.3: Jelly Bean
 • 4.4: KitKat
 • 5.0 and 5.1: Lollipop
 • 6.0 and 6.0.1: Marshmallow[4]
 • 7.0 and 7.1: Nougat
 • 8.0: Oreo

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Android Project Home
 2. There Are Now 1.3 Million Android Device Activations Per Day. TechCrunch (2012-09-05).
 3. Number of apps on Android Devices.
 4. Introducing new Android OS Marshmallow 6.0. Android Official. Iliwekwa mnamo 1 June 201.
Cite error: <ref> tag with name "ARMAN-4.0-on-x86" defined in <references> is not used in prior text.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]