Nenda kwa yaliyomo

Saa ya mkononi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tangazo la saa iliyotengenezwa na Mappin & Webb mwaka 1898.

Saa ya mkononi ni kifaa ambacho hubebwa au kuvalishwa mkononi ambapo hueleza muda.

Kuna saa za digitali na saa za mishale.

Siku hizi matumizi yake yamepungua kwa sababu kuna vifaa vingine, kama simu ya mkononi, ambavyo hufanya kazi ya kuonyesha wakati pia.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Dhana ya saa ya mkono ina historia ndefu toka wakati wa uzalishaji wa saa za mwanzo kabisa katika karne ya 16. Malkia Elizabeth I wa Uingereza alipokea saa ya mkono kutoka kwa Robert Dudley mnamo mwaka wa 1571.

Mwaka wa 1775 saa ilipatikana yenye uwezo wa kukaza kamani yake kwa nishati ya msuko suko wa mkono mtu akitembea na mpaka wa leo inatumika na watu wengi. Saa ya mkono ya zamani kabisa iliyopo hadi hivi sasa (iliyokuwa ikiitwa saa ya bangili) ilitengenezwa mwaka 1806. Mwanzoni saa za mkono zilikuwa zikivaliwa na wanawake tu, wakati wanaume walikuwa wakitumia saa za mfukoni hadi karne ya 20.

Saa za mkono zilianza kuvaliwa na wanaume wanajeshi mwisho mwa karne ya 19 kwa ajili ya kupanga vyema vita. Kampuni ya Garstin ya London ilipata hati miliki ya "Watch Wristlet" mwaka 1893, lakini walikuwa wakitengeneza saa miundo kama hiyo tangu miaka ya 1880. Maofisa wa Jeshi la Uingereza walianza kutumia saa za mkonononi wakati wa kampeni ya kijeshi ya kikoloni katika miaka ya 1880, kama vile wakati wa Vita ya Anglo-Burma ya 1885. Wakati wa Vita ya kwanza ya Makaburu, umuhimu wa kuratibu harakati za vikosi na kusawazisha mashambulizi dhidi ya Makaburu ulikuwa muhimu sana, na matumizi ya saa za mkono ulianza kuenea miongoni mwa maofisa wa kijeshi. Kampuni ya Mappin & Webb ilianza uzalishaji wa saa za wanajesho wakati huko Sudan mnamo mwaka 1898 na kuongeza kasi ya uzalishaji wakati wa Vita ya Pili ya Makaburu miaka michache baadaye. Katika bara la Ulaya kampuni ya Girard-Perregaux na kampuni nyingine za Uswisi zilianza kutengeneza saa za mkono za maofisa wa jeshi la Ujerumani mwaka 1880.

Kawaida ubora wa saa unahusishwa na mambo mbalimbali kama vile saa inavyoweza kuzuia maji. Shirika la Kimataifa la Usanifishaji (kwa kifupi ISO) limetoa vipimo maalum vya saa zinavyozuia maji.

Saa zaweza kugawiwa katika makundi mawili makuu kuzingatia kizazi; saa za zamani (analog) na saa za kisasa/za dijiti ambazo ni za kielektroni.

Pia zinaweza kugawiwa katika makundi saba kulingana na mtindo na utenda kazi:

  • saa za kujiendesha (automatiki) - saa zisizo hitaji betri
  • saa za kronogilafia (chronograph watches) - saa zijulikanazo kwa Kingereza kama "Stop-Watch" za kupimia mda mfupi hasa wakati tendo kama mbio zinafanyika
  • saa zisizo na mengi (minimalist watches) - saa zisizo na marembesho mengi
  • saa za quartz - saa zinazo tumia teknolojia ya quartz
  • saa za kimtindo - saa za kisanaa zinazolenga mvuto wa pekee
  • saa za fahari - saa zenye bei ghali mno zinazoundwa kwa kulenga matajiri na mara nyingi huendana na vitu vya fahari kama magari na simu
  • saa zinazotumia nishati ya jua
  • saa za wanariadha - saa za kisasa ambazo, mbali ya kueleza muda, pia zinapima mapigo ya moyo na mambo mengine muhimu ya kuzingatiwa na wanariadha wanapofanya mazoezi

Viungo za nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.