Nenda kwa yaliyomo

Chatu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Python)
Chatu
Chatu kaskazi Python sebae
Chatu kaskazi
Python sebae
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Oda ya chini: Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
Familia: Pythonidae (Nyoka walio na mnasaba na chatu)
Jenasi: Python
Daudin, 1803
Ngazi za chini

Spishi 10:

Chatu ni spishi za nyoka katika jenasi Python wa familia Pythonidae. Kwa sababu hawana sumu lazima waue mawindo yao kwa njia nyingine. Kwa hivyo huzongamea mwili wao kuzunguka kidari cha mawindo kisha kubana kwa nguvu ili kuzuia mawindo asipumue mpaka afe halafu hummeza mzima.

Kwa kawaida chatu ni miongoni mwa majoka makubwa ambayo upata mawindo yake kwa kuvizia au kutega katika njia wapitamo mawindo. Kwa kawaida chatu hukamata wanyama wadogo kiasi kama vile panya, sungura, kanga, mbwa, mbuzi na paa. Spishi kubwa kama chatu kaskazini zinaweza kumeza ndama wa wanyama wakubwa kama vile swala, nyumbu, pofu, kondoo na ng'ombe, na hata binadamu na watoto wake lakini kwa nadra tu. Kwa hivyo kiumbe huyu inaweza kuwa hatari kwa maisha ya viumbe hai wengine.

Chatu kulingana na maumbile yao wapo wa aina kuu mbili yaani wembamba na wanene. Chatu wembamba mara nyingi hupatikana hasa katika maeneo ya milimani na chatu wanene hupatikana na upendelea kuishi hasa katika maeneo ya bondeni.

Spishi za Afrika

Spishi za Asia

Picha

Marejeo

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chatu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.