Nenda kwa yaliyomo

Grigori Rasputin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha halisi ya Rasputin.

Grigori Yefimovich Rasputin (kwa Kirusi: Григо́рий Ефи́мович Распу́тин, 22 Januari 1869 - 30 Desemba 1916) alikuwa mkulima na mponyaji wa imani wa Urusi. [1] Hakuwa mtawa aliyeishi katika nyumba ya watawa, bali ni mhiji wa kidini. Alianza kupata sifa kama "mtu mtakatifu" katika mazingira ya Siberia akaendelea kuwa rafiki wa wakuu wa Kanisa la Kiorthodoksi.

Mnamo 1904 alifika katika mji mkuu wa Sankt Peterburg akakutana na wakuu wa jamii, watu kutoka tabaka la makabaila. Hatimaye aliweza kukutana hata na Tsar (mfalme) Nikolai II na malkia wake Aleksandra. Walimwomba amwombee mtoto wao Aleksei aliyekuwa na ugonjwa wa hemofilia (ugonjwa wa kutokwa damu; ulisababisha maumivu kwenye kinena na miguu kila alipoanguka) wakaona mtoto alipata nafuu akiombewa na Rasputin. Hivyo alifika kwenye nafasi ya kuwa mshauri wa kiroho kwa tsar na mke wake.[2] Malkia Aleksandra aliamini kwamba Rasputin ndiye mtu pekee ambaye anaweza kumponya mtoto wake kwa maombi yake.

Kwa sababu hiyo, Tsar na familia yake walianza kumwamini Rasputin zaidi na maamuzi muhimu juu ya siasa. Rasputin hakuunga mkono Tsar alipoamua kuiongoza nchi yake katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

Mnamo Agosti 1915, Tsar aliamua kuongoza jeshi la nchi mwenyewe, na kuchukua nafasi ya binamu yake Mtemi Nikolai. Wanasiasa wengi wa Urusi na wakuu walipata wasiwasi sana juu ya ushawishi mkubwa wa Rasputin. Wakati Tsar alikuwa pamoja na wanajeshi wake, Alexandra na Rasputin walichukua maamuzi yaliyoongeza wasiwasi katika serikali. Walipendekeza kwa Tsar kubadilisha mawaziri kadhaa na kuteua wengine waliounga mkono amani.

Hivyo wapinzani wa Rasputin waliamua kumwondoa katika mazingira ya tsar kwa kumwua.

Usiku wa Desemba 30, 1916, Rasputin alipigwa risasi mara mbili na Felix Yusupov aliyekuwa kijana wa familia ya tsar. Wauaji walimtupa katika mto Neva mjini Sankt Peterburg.[3]

  1. Maria Aprelenko (2011). "Prominent Russians: Grigory Rasputin". Russiapedia. Iliwekwa mnamo 16 Novemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. http://russiapedia.rt.com/prominent-russians/history-and-mythology/grigory-rasputin Archived 13 Novemba 2021 at the Wayback Machine. Prominent Russians: Grigory Rasputin
  3. http://russiapedia.rt.com/prominent-russians/history-and-mythology/grigory-rasputin Archived 13 Novemba 2021 at the Wayback Machine. Prominent Russians: Grigory Rasputin
Picha ya Grigori Rasputin (1910).
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.