Gaetano wa Thiene
Mandhari

Gaetano wa Thiene (Vicenza, 1 Oktoba 1480 – Napoli, 7 Agosti 1547), alikuwa padri wa Italia ambaye alichangia sana uamsho wa Kanisa wakati wa Urekebisho wa Kikatoliki hasa kwa njia ya aina mpya ya utawa aliyoianzisha, maarufu kwa jina la Wateatini, aliowaachia jukumu la kufuata mtindo wa maisha ya Mitume wa Yesu. Kwa shirika hilo alifungua njia kwa mashirika mengine kama la Wajesuiti, la Wabarnaba na la Wasomaski.
Huko Napoli alijitosa katika matendo ya huruma, hasa kwa ajili ya waliopatwa na magonjwa wasiotibika, na kuhamasisha vyama kwa ajili ya malezi ya Kikristo ya walei [1].
Alitangazwa na Papa Urban VIII kuwa mwenye heri tarehe 8 Oktoba 1629, halafu Papa Klementi X alimtangaza mtakatifu tarehe 12 Aprili 1671.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- Masomo ya Breviari - Sikukuu za Bwana, za Bikira Maria na za Watakatifu - Ndanda Mission Press 1978, uk 273-275
- John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 271
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Catholic Encyclopedia: St Cajetan
- Patron Saints Index: Saint Cajetan Ilihifadhiwa 10 Mei 2013 kwenye Wayback Machine.
- Ilihifadhiwa 29 Machi 2019 kwenye Wayback Machine.
- Statue of St Cajetan in St Peter's Basilica
- Ilihifadhiwa 3 Novemba 2006 kwenye Wayback Machine. Maisha yake kwa Kihispania
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |