Wateatini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kanisa la Wateatini mjini Roma, Sant'Andrea della Valle.

Wateatini (kwa Kiingereza jina kamili la shirika ni: Congregation of Clerks Regular of the Divine Providence, kifupi "C.R.") ni utawa wa kikleri wa Kanisa Katoliki ulioanzishwa na Gaetano wa Thiene, Paolo Consiglieri, Bonifacio da Colle, na Giovanni Pietro Carafa (ambaye akawa Papa Paulo IV).

Aina hiyo mpya ya shirika likawa kielelezo kwa mengine mengi, kama vile Wajesuiti, Wabarnaba, Wasomaski n. k.

Lengo kuu la shirika hilo lilukuwa kurudisha wenye daraja takatifu kwenye uadilifu.

Kati ya watakatifu wa shirika hilo, mbali ya mwanzilishi, wapo Andrea Avellino, Yosefu Maria Tomasi. Wapo pia wenye heri kadhaa.

Kadiri ya Annuario Pontificio, tarehe 31 Desemba 2008 Wateatini duniani walikuwa 189 katika nyumba 33 houses. Kati yao 133 walikuwa mapadri.

StPetersDomePD.jpg Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wateatini kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.