Kenya (mlima)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mlima Kenya

Mlima Kenya ndio mlima mrefu kuliko yote nchini Kenya. Mlima huu ambao hasa wenyeji waliuita Kirinyaga, una urefu wa mita 5,199. Mlima huu unatokana na volkeno iliyozimika ikikadiriwa ya kwamba mlipuko wake wa mwisho ulitokea mnamo miaka milioni 2.6 hadi 3.1 iliyopita.

Vilele vyake vya juu vinaitwa Batian (5,199 m), Nelion (5,188 m) na Lenana (4,985 m). Kuna barafuto nane mlimani lakini zinapungua kila mwaka kutokana na kupanda kwa halijoto duniani na kupungukiwa kwa usimbishaji kwa sababu ya kukatwa kwa miti mingi.

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kenya (mlima) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.