Shirika la Huduma kwa Wanyama Pori ya Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kenya Wildlife Service)
Huduma ya Wanyamapori Kenya,njia ya Kupanda Mlima - lango la Hifadhi
Huduma ya Wanyamapori Kenya,njia ya Kupanda Mlima - lango la Hifadhi

Shirika la Kenya la Wanyama Pori (KWS - Kenya Wildlife Service) lilianzishwa mwaka 1990. Inasimamia uasilia na viumbe hai wa nchi, ikilinda na kuhifadhi flora na fauna.

KWS inasimamia mbuga za wanyama za kitaifa na hifadhi nchini Kenya. Fedha zinazokusanywa kama ada ya kiingilio hutumika kusaidia uhifadhi wa mimea na wanyama ndani ya hifadhi au mbuga.

Mbuga za Kitaifa na za Hifadhi[hariri | hariri chanzo]

Kenya ina mbuga na hifadhi 35 teule za kitaifa:

Mipango ya Uhifadhi[hariri | hariri chanzo]

KWS inaendesha mipango maalum kusaidia viumbe na makazi ya Kenya ambayo yako kwenye hatari hasa. Wana mipango ya uhifadhi wa sehemu za chemchemi na misitu,na miradi maalum ya tembo na kifaru kusaidia kuwaokoa kutoka kwa wawindaji. Hirola, ambayo iko katika hatari ya kupotea, pia inafuatiliwa.

Ndani ya KWS kuna huduma kadhaa, kila moja ikiwajibika kwa eneo tofauti la kazi:

Huduma ya Wanyama Pori ya Jamii[hariri | hariri chanzo]

Hili tawi la KWS hufanya kazi nje ya hifadhi za taifa. Wao badala hufanya kazi katika maeneo kama vile kanda za wanyamapori, na kufundisha jamii wanaoishi huko kuhamasisha uhifadhi na kuchunga rasilimali zao.

Huduma za Usalama[hariri | hariri chanzo]

Kazi ya huduma hii ni kuondoa uwindaji katika hifadhi za kitaifa, na kukomesha biashara haramu.

Huduma za Matibabu ya Wanyama[hariri | hariri chanzo]

Huduma hii huhakikisha kuwa afya ya kuzaliana ya wakazi wa aina inazingatiwa kote nchini.

Mafunzo[hariri | hariri chanzo]

KWS ina kituo cha mafunzo mjini Naivasha. Watumishi wa KWS hufundishwa hapa, na pia mafunzo kwa wanafunzi wa nje wa ikolojia na utalii.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

KWS inendesha vituo kadhaa vya elimu:

  • Nairobi Safari Walk
  • Kituo cha Elimu cha Nairobi
  • Kituo cha Elimu cha Ziwa Nakuru
  • Kituo cha Elimu cha Tsavo Mashariki
  • Kituo cha Elimu cha Tsavo Magharibi

Hizi ziko ndani ya Hifadhi za Taifa, na huendesha mipango ya kuhamasisha watu kuhudumia na kulinda mazingira yao. Imelengwa kwa wananchi, hasa makundi ya shule, lakini ni wazi kwa mtu yeyote.

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]