Nenda kwa yaliyomo

Masai Mara

Majiranukta: 1°29′24″S 35°8′38″E / 1.49000°S 35.14389°E / -1.49000; 35.14389
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mandhari ya Kimasai Mara
Hifadhi ya Taifa ya Masai Mara
Masai Mara iko katika eneo la Bonde la Ufa
MahaliKenya, Kaunti ya Narok
Nearest cityNyeri
Coordinates

1°29′24″S 35°8′38″E / 1.49000°S 35.14389°E / -1.49000; 35.14389{{#coordinates:}}: cannot have more than one primary tag per page

Eneo1,510 km²
Kuanzishwa1974
Mamlaka ya utawalaTrans-Mara and Narok County Councils

Masai Mara (pia: Maasai Mara) ni hifadhi kubwa ya wanyamapori katika Kaunti ya Narok, Kusini Magharibi mwa Kenya, ambayo ni muendelezo wa Kaskazini wa mbuga ya hifadhi ya Serengeti iliyoko nchini Tanzania.

Jina linatokana na jamii ya Wamaasai (wenyeji wa tangu jadi wa eneo hilo) na Mto Mara unaoigawa. Ni maarufu kwa wingi wa wanyama wake wa pekee na uhamaji wa pundamilia, swala wa aina ya Thomson, na kongoni kutoka Serengeti kila mwaka kuanzia Julai hadi Oktoba, uhamaji mkubwa sana uitwao "Uhamaji Mkuu".

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Hifadhi ya Wanyamapori ya Kitaifa ya Masai Mara ina upana wa kilomita 1530. Ndiyo sehemu ya Serengeti iliyo upande wa Kaskazini zaidi yenye upana wa jumla ya kilomita za mraba 25,000. Upande wa Kusini imepakana na mbuga ya wanyama ya Serengeti, na upande wa magharibi na mharara wa Siria na upande wa Kaskazini Mashariki na Magharibi imepakana na maeneo ya ufugaji.

Kiwango cha mvua katika mazingira hayo huongezeka kuanzia kusini-mashariki hadi magharibi, japo hubadilika kiwakati kutoka eneo moja hadi lingine na ni ya misimu miwili. Mito ya Sand, Talek na Mara ndiyo mito mikubwa ambayo hutoa maji kwenye hifadhi ya mbuga hii. Vichaka na miti iliyomea kwenye kingo za mito hufunika miteremko na vilele vya milima.

Kimsingi mandhari ya hifadhi hii ni nyasi iliyo wazi na mito. Eneo la Kusini Magharibi kuna vichaka vya aina mbalimbali ya miti ya aina ya mwangate. Upande wa mpaka wa magharibi kuna harara (genge) la Esoit Oloololo la Bonde la Ufa, na wanyamapori wanapatikana eneo hili kwa wingi kwa sababu chemchemi ya maji hupatikana kwa urahisi na hakuna usumbufu wa watalii. Mwisho wa mpaka wa Mashariki ni kilomita 224 kutoka Nairobi, kwa hiyo, upande wa mashariki ndio hutembelewa na watalii sana.

Wanyamapori wa Masai Mara

[hariri | hariri chanzo]

Kongoni, pundamilia na swala wa aina ya Thomson huhamia hifadhi ya mbuga ya Mara kutoka sehemu tambarare za Serengeti hadi nyanda za Kusini na za Loita katika maeneo ya wachungaji kuelekea Kaskazini Magharibi Kuanzia Julai hadi Oktoba ama baadaye. Makundi hayo matatu pia hupatikana kwenye hifadhi ya mbuga ya Mara.

Wanyama wote wa kundi la "Tano Kubwa" wanapatikana Masai Mara, ingawa idadi ya vifaru weusi inapungua, huku kukiwa na jumla ya vifaru 37 tu katika mwaka wa 2000. Viboko hupatikana wakiwa kwenye makundi makubwa kwenye mito ya Masai Mara na Talek. Duma pia hupatikana, ingawa idadi yao inapungua kwa kasi mno, hususan kutokana na usumbufu wa watalii na uwindaji wao wa mchana. Kama ilvyoelezwa hapo juu, sehemu tambarare kati ya mto Mara na harara ya Esoit Oloololo ndiyo sehemu nzuri ya kusimama ili kuweza kuwaona wanyamapori vizuri hususan simba na duma.

Kama ilivyo kwenye mbuga ya Serengeti, kongoni ndio wengi zaidi katika hifadhi ya Masai Mara, na idadi yao inakadiriwa kuwa mamilioni. Karibu kila mwaka mwezi wa Julai wanyama hao huhamia eneo la Kaskazini kwa wingi kutoka Serengeti wakitafuta lishe, na hurudi upande wa Kusini katika mwezi wa Oktoba. Uhamaji mkubwa ni mojawapo ya matukio asilia ya kuvutia ulimwenguni kote, unaohusisha wanyama wala majani, kongoni 1,3000,000, swala 360,000 na pundamilia 191,000. Wanyama hao ambao huhama hufutwa kupitia kwa njia yao mviringo na kundi la wanyama walanyama, kama vile simba na fisi.

Paa wengine wengi wanapatikana hapa, wakiwemo swala wa aina ya Thomson na Gant, swalapala na kongoni. Kuna pundamilia wengi kwenye hifadhi ya mbuga hiyo. Nyanda hizo ni makazi ya twiga wa aina tofauti ya Masai Mara pamoja na twiga wa kawaida. Paa mkubwa wa aina ya Roan na mbweha mwenye masikio kama ya popo anayetembea usiku wanaonekana pia kwenye mipaka ya mbuga hiyo. Masai Mara ni kituo kikubwa cha utafiti wa fisi mwenye mabaka. Kuongezea ni kwamba kuna zaidi ya aina 450 ya ndege wa msituni, ikiwa ni pamoja na mwewe, kongoti, ndege wadogo, hondohondo, korongo wenye shungi kichwani, tai, na vipanga wafupi wa Kiafrika.

Hifadhi ya mbuga ya wanyama ya Masai Mara inasimamiwa na Baraza la mji wa Narok na Mara Conservancy (chini ya mkataba na Baraza la Trans-Mara), shirika lisilo la faida lililoundwa na Wamaasai, na lenye vitengo vinavyozuia usasi haramu. Hifadhi ya Masai Mara ni eneo linalosimamiwa na shirika la Group Ranch Trust la jamii ya Masai Mara ambao pia wana askari misitu wao ambao hushika doria kwenye hifadhi hiyo. Wanyapori huzurura kwenye hifadhi hiyo bila ya kizuizi chochote na kwenye mazingira ya wanyamapori yaliyotunzwa.

Mbuga za wanyama huiletea nchi ya Kenya fedha za kigeni. Kufikia Oktoba mwaka 2009 ada za kiingilio zilikuwa ni dola za Marekani 60 kwa watu wazima na dola 30 kwa watoto wageni wasio Wakenya. [1] Kuna mikahawa ya kulala na kambi nyingi za mahema kwa watalii wanaozuru mbuga hiyo na maeneo ya mipaka yake. Watalii / wageni hugharimia matumizi yao isipokuwa kama kulikuwa na mpango awali wa matumizi yao.

Mikahawa ya kulala na kambi zinazopatikana kwenye mikahawa hiyo ni pamoja na Mara Reserve Serena, Gavana wa kambi, Keekorok, na Sarova Mara. Katika eneo la hifadhi kuna Royal Mara Safari Lodge, kambi ya hema ya Siana Springs, Mara Sopa, Elephant Pepper, Mara, Simba, na kambi ya Sekenani. Ada ya kupiga kambi ni dola za Marekani 25 kwa kila usiku.

Kiwanja cha ndege cha Mara Serena, kiwanja cha Musiara na kile cha Keekorok vipo katika eneo la uhifadhi wa Mara. Viwanja vya ndege vya Mara Shikar, Kichwa Tembo na Airport Ngerende vinapatikana katika eneo la Uhifadhi la Masai Mara.

Matangazo ya vyombo vya habari

[hariri | hariri chanzo]

Big Cat Diary ya Televisheni ya BBC imepiga picha kwenye mbuga hiyo na eneo la Uhifadhi wa Masai Mara na inaonyesha matukio kutoka eneo la mbuga hiyo la Musiara Marsh na Leopard George na sehemu za uhifadhi za mtini.

Hifadhi ya mbuga ya Mara ina tovuti ambayo kazi yake ni kutoa maelezo zaidi kuhusu mimea na wanyama, ramani, historia na utamaduni wa Wamaasai, uhamaji wa kongoni, habari zinazochipuka na matukio, ada ya kiingilio na malazi. Kuna fedha zimengwa bila ya upendeleo wowote kuboresha Maasai Mara kama kivutio cha utalii.

Maasai Mara katika hatari

[hariri | hariri chanzo]

Kwa mujibu wa utafiti mpya Mbuga ya Kitaifa ya Maasai Mara inapoteza spishi za wanyama kwa kasi ambayo inawatia wasiwasi wanasayansi.

Matokeo yaliyochapishwa kwenye Juzuu la British Journal of Zoology (Ilri Scientific Paper_Dynamics of Mara-Serengeti Ungulates in Relation to Land Use Changes) yananasibisha kutoweka kwa spishi hizo na ongezeko la makazi ya binadamu ndani na karibu na mbuga hiyo.

Makala iliyokuwa kwenye tovuti ya Taasisi ya Kimatifa ya Utafiti wa Wanyama (ILRI) ilisema kuwa "Utafiti huo unatoa ushahidi mpana hadi wa leo kuhusu kupungua kwa idadi ya wanyama wenye kwato kwenye mbuga ya Mara na jinsi hali hii inavyohusishwa na ongezeko la haraka la idadi ya watu katika maeneo yanayopakana na mbuga hiyo."

ILRI ilifanya utafiti huu kati ya mwaka 1989 na 2003. Utafiti huo uliofadhiliwa na Mfuko wa Wanymapori wa kwa ajili ya Mazingira (WWF), ulifuatilia wanyama wenye kwato kila mwezi kwa kipindi cha miaka 15.

Kulingana na utafiti huu, spishi sita pamoja na twiga, paa, ngiri, topis na bata wa majini wapungua sana kwenye mbuga hiyo kwa kasi ya kutia wasiwasi.

Utafiti huo unasema kuwa idadi ya wanyama walioangamia ni kubwa kiasi cha asilimia 95 cha twiga, asilimia 80 ya ngiri, asilimia 76 ya kongoni na asilimia 67 ya swalapala.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Utalii nchini Kenya (KTF) idadi ya nyumba zinazojengwa kwenye mbuga hiyo zitakuwa zaidi ya idadi ya wanyama kwa kipindi cha miaka 20.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Julie Ward, mpigapicha wa wanyamapori aliyeuawa katika mbuga ya Masai Mara mwaka 1988
  1. Conservancy wa Mara - Park fee Archived 2 Desemba 2009 at the Wayback Machine. 3 Novemba 2009

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: