Bata

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bata
Bata domo-njano
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Anseriformes (Ndege kama bata)
Familia: Anatidae (Ndege walio na mnasaba na bata)

Mabata ni ndege wa maji wa familia ya Anatidae wenye midomo mifupi na mipana na miguu yenye ngozi kati ya vidole. Manyoya yao huwa na uwezo bora wa kufukuza maji kwa msaada wa mafuta maalumu. Mabata ndiyo moja ya familia za ndege ambazo spishi zao zina uume, kwa sababu mabata wanapandana majini tu.

Ndege hawa wana rangi mbalimbali. Spishi kubwa hutafuta chakula aghalabu ardhini au kwa maji machache. Spishi ndogo nyingine hula mimea ya maji na huzamia kichwa chao tu, nyingine huzamia kabisa ili kukamata samaki, wanyamakombe au mimea ya maji, lakini spishi kadha hutafuta chakula ardhini. Hujenga matago yao ardhini, juu ya mwamba, ndani ya shimo la miti au ndani ya pango la sungura, mhanga, k.y.k.

Manyoya ya spishi kadha hupendwa sana kama kijazo cha mito, mifarishi, mafuko ya kulalia na makoti. Spishi nyingi za mabata hutumika kama chakula.

Wataalamu hawakubaliana kuhusu uainisho wa mabata ndani ya familia yao. Kuna miainisho mbalimbali na mmoja tu unaonyeshwa hapa:

Yaliyomo

[hariri] Dendrocygninae: Mabata-miti

Bata-miti uso-mweupe

Mabata wenye miguu mirefu ambao wanafanana na mabata bukini. Jenasi moja itokeayo kila mahali pa kufaa nchini kwa tropiki:

[hariri] Thalassorninae: Kotwe

Wana mnasaba na Dendrocygninae, lakini wanafanana na familia ndogo Oxyurinae. Jenasi moja kwa Afrika:

[hariri] Anserinae: Mabata-maji na mabata bukini

Bata-maji domo-fundo

Spishi 27 za mabata wakubwa ndani ya jenasi 7 ambazo zinatokea kanda za halijoto wastani hasa kaskazini mwa ikweta lakini spishi chache kusini mwa ikweta (spishi kadhaa, kama bata-maji domo-fundo, zimewasilishwa kwa Afrika):

[hariri] Stictonettinae: Bata madoadoa

Bata madoadoa

Jenasi moja kwa Australia ambayo ilikuwa imeainishwa zamani ndani ya Oxyurinae, lakini anatomia yake ionyesha mnasaba na Anserinae:

[hariri] Plectropterinae: Bata bukini bawa-kijani

Jenasi moja kwa Afrika ambayo ilikuwa imeainishwa zamani kama 'bata anayetua', lakini iko karibu zaidi na Tadorninae:

[hariri] Tadorninae: Mabata-shimo

Bata bukini wa Misri

Jamii hii ya mabata makubwa wanaotokea mara nyingi nchini kavu ni kati ya Anserinae na Anatinae. Juzijuzi wataalamu wameainisha jenasi 10 na spishi 23 (moja imekwisha labda) ndani ya familia ndogo hii, nyingi zaidi kutoka kusini mwa ikweta:

[hariri] Anatinae: Mabata wachovya na wazamaji na moa-nalo

Bata bawa-kijani

Jamii ya mabata wachovya ambao wanatokea sehemu zote duniani ilikuwa imeainishwa kwa jenasi mbili tu, lakini ina jenasi 8 sasa na spishi 55:

Bata domo-jembamba

Jamii ya mabata wazamaji ambao wantokea sehemu zote duniani ina spishi 16 ndani ya jenasi 3. Marmaronetta ilikuwa imeainishwa zamani miongoni mwa mabata wachovya lakini inaainishwa hapa sasa.

Jamii ya moa-nalo (jina kwa Kihawaii) ni ya pekee. Mabata hawa walitokea Hawaii lakini wamekwisha sasa. Walikuwa wakubwa sana na domo nene sana na walifanana na mabata bukini ambao hawakuweza kuruka angani. Walikuwa na mnasaba na jenasi Anas.

[hariri] Merginae: Mabata-bahari

Bata-domomeno kidari-chekundu

Familia ndogo hii ina spishi 20 (moja au mbili zimekwisha). Spishi nyingi zaidi zinatokea kaskazini mwa ikweta, lakini kuna spishi mbili za Mergus kusini mwa ikweta.

[hariri] Oxyurinae: Mabata mkia-ngumu

Bata kichwa-cheupe

Jamii ndogo ya mabata iliyo na spishi 8 ndani ya jenasi 4:

[hariri] Spishi za Afrika