Ziwa Burigi
Mandhari
Burigi ni ziwa la Tanzania kaskazini-magharibi, katika mkoa wa Kagera. Linapakana na wilaya tatu za mkoa huo yaani Muleba, Karagwe na Biharamulo. Hata hivyo halijabahatika kupata barabara ya kuliunganisha moja kwa moja na wilaya hizo.
Ziwa hilo lina aina mbalimbali za samaki kama vile kambale, kamongo, bauta (sato), bugege na buyamba (dagaa). Ziwa hilo limegawiwa kati ya hifadhi ya samaki na maeneo ya wananchi kuvua samaki japo hakuna mipaka rasmi ndani ya ziwa. Pia ndani ya ziwa hilo kuna wanyama aina ya kiboko.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]2°07′23″S 31°18′54″E / 2.123°S 31.315°E
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ziwa Burigi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |