Nenda kwa yaliyomo

Vikta wa Marseille

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu yake huko Nooit Gedagt (Uholanzi).

Vikta wa Marseille (alifariki Marseille, Ufaransa, 21 Julai 292 hivi) alikuwa askari wa jeshi la Roma ya Kale aliyekuwa chini ya Morisi Mtakatifu[1].

Kufuatana na mapokeo ya karne ya 4 kikosi chake kilijumlisha wanajeshi Waafrika kutoka Misri ya kusini na Nubia waliotumwa Ulaya wakati wa Kaisari Maximiano wa Roma. Wengi wao walikuwa Wakristo. Katika mapokeo ya sanaa ya Kikristo walichorwa kama Waafrika weusi.

Huko Agaunum (leo Saint-Maurice-en-Valais), karibu na mto Rhone, katika eneo la Uswisi wa leo, walipewa amri ya kujiandaa kwa mapigano dhidi ya waasi na kabla ya mapigano kutoa sadaka kwa Kaisari aliyeheshimiwa kama mungu mmojawapo. Wakristo hao walikataa kutoa sadaka hiyo. Kaisari alipopata habari hii akakasirika akatoa amri kuua kila askari wa kumi katika kikosi. Wakristo walipoendelea kukataa amri ilirudiwa hatimaye karibu kikosi chote kiliuawa pamoja na kiongozi chake Morisi.

Vikta ni kati ya wachache walionusurika ila akaja kuuawa baadaye huko Marseille.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini[2].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Henry Wace, A Dictionary of Christian Biography, Literature, Sects and Doctrines (1880), 439.
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/63875
  3. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.