Morisi Mtakatifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Morisi Mtakatifu katika sare ya kijeshi. Sanamu hiyo ipo katika kanisa kuu la Magdeburg, Ujerumani.
Morisi kama mwanajeshi kwenye nembo ya mji wa Buederich, Ujerumani.

Morisi Mtakatifu (pia: Maurice, Mauritius) alikuwa kiongozi wa kikosi cha Thebi katika jeshi la Roma ya Kale.

Kifodini chake[hariri | hariri chanzo]

Kufuatana na mapokeo ya karne ya 4 kikosi hicho kilijumlisha wanajeshi Waafrika kutoka Misri ya kusini na Nubia waliotumwa Ulaya wakati wa Kaisari Maximiano wa Roma. Wengi wao walikuwa Wakristo.

Katika eneo la Uswisi wa leo walipewa amri ya kujiandaa kwa mapigano dhidi ya waasi na kabla ya mapigano kutoa sadaka kwa Kaisari aliyeheshimiwa kama mungu mmojawapo. Wakristo hao walikataa kutoa sadaka hiyo. Kaisari alipopata habari hii akakasirika akatoa amri kuua kila askari wa kumi katika kikosi. Wakristo walipoendelea kukataa amri ilirudiwa hatimaye kikosi chote kiliuawa pamoja na kiongozi chake Morisi.

Heshima baada ya kifo[hariri | hariri chanzo]

Morisi pamoja na askari wa kikosi cha Thebi waliheshimiwa kama watakatifu na wafiadini Wakristo.

Katika mapokeo ya sanaa ya Kikristo walichorwa kama Waafrika weusi.

Miji mbalimbali ya Uswisi na Ujerumani walitumia na wanatumia picha za Morisi au watakatifu wengine wa Kikosi cha Thebi katika nembo zao. Mara nyingi kama mji wa Ulaya una picha ya mtu mweusi katika nembo yake hii inammaanisha Morisi Mtakatifu au wenzake.

Morisi aliheshimiwa hasa kama kielelezo cha mwanajeshi bora.

Mji wa Sankt Moritz (Saint Maurice) nchini Uswisi unabeba jina lake.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]