Nenda kwa yaliyomo

Urani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Urani (uranium)
Mtapo wa urani
Mtapo wa urani
Jina la Elementi Urani (uranium)
Alama U
Namba atomia 92
Mfululizo safu Metali
Uzani atomia 238.0289
Valensi 2, 8, 18, 32, 21, 9, 2
Densiti 19.1  g·cm³
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 1405.3 K (1132.2 °C)
Kiwango cha kuchemka 4404 K (4131 °C)
Asilimia za ganda la dunia 3 · 10-4 %
Hali maada mango
Uraniamu

Urani (kwa Kiingereza uranium) ni elementi katika mfumo radidia yenye alama U. Namba atomia ni 92 na uzani atomia ni 238. Atomi yake ina protoni 92 na elektroni 92.

Jina limechaguliwa kutokana na sayari iliyoitwa Uranus kwa kumbukumbu ya mungu mmojawapo wa Dola la Roma.

Urani ni metali nururishi. Isotopi za kawaida katika urani ni urani-238 na urani-235.

Urani ina uzani atomia wa juu kati ya elementi zote zinazotokea kiasili maana yake masi ya atomu yake ni kubwa zaidi. Hata hivyo densiti yake si juu zaidi hivyo mchemraba wa cm³ 1 wa urani ni mwepesi kuliko mchemraba wa cm³ 1 wa dhahabu.

Urani ni metali nyeupe nururishi katika mfululizo wa aktinidi. Isotopi yake 235U ni dutu asilia pekee inayoweza kuwa na mmenyuko mfululizo wa kinyuklia.

Kwa sababu hiyo hutumiwa katika tanuri nyuklia na katika silaha za nyuklia kwa ajili ya vita. Bomu la nyuklia la kwanza lililorushwa juu ya Hiroshima lilitengenezwa kwa urani.

Umuhimu wa kiuchumi

[hariri | hariri chanzo]

Ikiwa ni metali nururishi pekee inayopatikana duniani kiasili hutumiwa kwa utengenezaji wa umeme katika tanuri nyuklia. Takriban asilimia 10 ya umeme duniani hutengenezwa kwa njia hii, katika nchi kadhaa ni sehemu kubwa ya umeme[1].

Mwanzoni mwa upatikanaji wa teknolojia hiyo katika karne ya 20 kulikuwa na matumaini makubwa ya kuwa italeta umeme nafuu kwa watu wote hasa tangu ilitambuliwa ya kwamba akiba za makaa mawe na mafuta ya petroli zitakwisha. Ila tu matatizo ya takataka nyuklia na ajali hatari za tanuri nyuklia yalichelewesha maendeleo ya matumizi yake. Vilevile maendeleo ya uzalishaji wa nishati mbadala kama vile umemejua au umeme wa upepo yalileta mitazamo mipya.

Tena upatikanaji wa urani yenyewe ni tatizo kwa sababu akiba za urani duniani zinazofaa kwa uchimbaji rahisi kiuchumi hukadiriwa kudumu kwa miaka 50-100 pekee.


  1. The Database on Nuclear Power Reactors, tovuti ya IAEA, ilitazamiwa Machi 2019
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Urani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.